Gesi miminika : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Methanier aspher LNGRIVERS.jpg|300px|thumb|Meli za kubeba gesi miminika mara nyingu hutambuliwa kutokana na matangi ya mviringo ]]
[[File:Gesi miminika chanzo - mteja.png|thumb|300px|Njia ya gesi miminika kutoka chanzo hadi mteja]]
'''Gesi miminika''' (kwa [[Kiingereza]]: ''Liquefied Natural Gas''; [[kifupi]]: ''LNG'') ni [[gesi asilia]] katika hali ya [[kiowevu]] au miminika. Ni [[dutu]] safi isiyo na [[rangi]] na isiyo na [[sumu]],<ref>"[http://naturalgas.org/lng/ Focus on LNG]" ''Naturalgas.org'', iliangaliwa 2019</ref> inayotengenezwa kwa kupoza [[gesi asilia]] hadi [[nyuzi joto]] -160[[ºC]] hadi kiwango ambacho inakuwa kimiminika. Mchakato huo hurahisisha usafirishaji wenye ufanisi wa gesi asilia kwa kutumia [[barabara]] ([[Lori|malori]]) au [[bahari]] ([[meli]]).<ref>"[https://lngfacts.org/about-lng/what-is-lng/ What is LNG]" ''Center for Liquified Natural Gas'', iliangaliwa Juni 2019</ref> Sababu kuu ya kupoza gesi ni, gesi miminika ina [[ujazo]] mdogo mara 600 kuliko gesi asilia ikiwa katika hali ya kawaida.<ref>"[http://www.naturalgas.org/lng/lng.asp Liquified Natural Gas (LNG]" ''NaturalGas.org'', retrieved 13 February 2012.</ref>
 
==Uzalishaji==
[[Asilimia]] kubwa ya gesi asilia hukatama kwenye chanzo na kusafirishwa kwa [[bomba|mabomba]] baada ya kuisafisha hadi kufikia hali ya [[methani]] safi kiasi<ref>[http://naturalgas.org/naturalgas/transport/ The Transportation of Natural Gas] ''Naturalgas.org'', iliangaliwa 2019</ref>. Pasipo mabomba ni muhimu kupunguza [[ujazo]] wa gesi hii ili kuisafirisha ama kwa meli au kwa malori.<ref>"[http://www.lngfacts.org/About-LNG/Overview.asp Overview-About LNG]" ''Center for Liquified Natural Gas'', retrieved 13 February 2012.</ref>
 
Hadi [[mwaka]] [[2012]], [[duniani]] kote kulikuwa na vituo 20 vya kuzalisha na kusafirisha nje gesi miminika, vituo 63 vya kuingiza gesi miminika ndani ya nchi, na takriban meli 300 za kubeba gesi ya kimiminika zote zikiwa na uwezo wa kubeba [[tani]] za [[meta]] [[milioni]] 750 za gesi ya kimiminika kila mwaka. Kiasi hikihicho kinategemewakinatarajiwa kuongezeka sana kwa kipindi cha miaka kumi ijayo kutokana na umaarufu unaoongezeka wa chanzo hikihicho safi cha kuwashia [[moto]].<ref>"[http://lnglicensing.conocophillips.com/EN/about/whatis/Pages/index.aspx What is LNG?]" ''ConocoPhillips'', retrieved 13 February 2012.</ref>
 
==Uchumi==
Ujengaji wa mitambo ya gesi miminika unahitaji [[mtaji]] mkubwa na yenye madeni makubwa.<ref>"[http://in.reuters.com/article/2012/09/19/us-eastafrica-gas-idINBRE88I0OG20120919 Analysis: East Africa risks missing LNG boom]" ''Reuters'', 19 September 2012.</ref> Lakini wakati gesi miminika ina gharama kiasi kuizalisha, maendeleo ya teknolojia yanapunguza gharama hizo zinazotokana na kuifanya kimiminika na kuirudisha tena katika hali yake ya gesi asilia.<ref>"[http://www.naturalgas.org/lng/lng.asp Liquified Natural Gas (LNG]" ''NaturalGas.org'', retrieved 13 February 2012.</ref> Chapisho la BP World Energy Outlook lilitabiri mnamo mwaka [[2012]] kwamba [[biashara]] ya gesi miminika itakua kwa haraka maradufu kama ulivyokua haraka uzalishaji wa gesi asilia duniani, yaani kwa kiwango cha asilimia 4.4 kwa mwaka.<ref>"[http://www.bp.com/liveassets/bp_internet/globalbp/globalbp_uk_english/reports_and_publications/statistical_energy_review_2011/STAGING/local_assets/pdf/2030_energy_outlook_booklet.pdf World Energy Outlook 2030]" ''BP'', retrieved 13 February 2012.</ref>
 
=Marejeo=