Waraka wa kwanza kwa Wakorintho : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
'''Barua ya kwanza kwa Wakorintho''' ni kati ya [[vitabu]] 27 vya [[Agano Jipya]] katika [[Biblia ya Kikristo]]
 
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya [[maendeleo]] ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
==Mazingira==
Kutoka [[Korintho]] ([[mji]] wa [[Ugiriki]]) habari za kusikitisha zilimfikia [[Mtume Paulo]] akiwa [[Efeso]] (pengine [[mwaka]] [[57]]): katika [[Kanisa]] hilo ambalo alilianzisha na kulipenda sana kulikuwa na [[shaka]] kuhusu [[imani]], ma[[farakano]], [[upinzani]] wa [[Wakristo wa Kiyahudi]] dhidi yake, na ma[[kwazo]].
 
Kilichohatarisha zaidi [[jumuia]] hiyo ni [[karama]] mbalimbali ambazo hao Wakristo wachanga walizijali mno na hatimaye wakajivunia kuwa nazo.
 
Vilevile walivutiwa kumfuata [[mtu]] kama [[Apolo]], mwenye [[ujuzi]] na [[ufasaha]] mkubwa, mambo yaliyopendwa sana na [[Wagiriki wa kale]].
 
Ilimbidi Paulo arekebishe [[hali]] hiyo ili kuokoa hasa [[umoja wa Kanisa]] na [[heshima]] kwa [[Kiongozi|viongozi]] wake halali.
 
Basi mwaka mzima akawa na mahangaiko kwa wafuasi wake wa Korintho akawaandikia walau barua [[nne]] au [[tano]], ingawa sisi tunazo [[mbili]] tu; pengine sehemu za baadhi yake zimeshonwa ndani ya [[2Kor]].
 
==Mpangilio==
Mpangilio wa barua ya kwanza una [[salamu]] na [[shukrani]], halafu [[hukumu]] juu ya matatizo ya Wakristo hasa kufarakana (1Kor 1:10-16; 2:1-4:16), [[Uzinifu|kuzini]] na kushtakiana [[Mahakama|mahakamani]] (1Kor 5-6).
 
Baada ya hapo akaanza kujibu maswali yao mbalimbali: kuhusu [[ndoa]] na [[useja]] (1Kor 7), [[nyama]] zilizotolewa [[sadaka]] kwa [[miungu]] (1Kor 8:1-11:1), mwenendo katika [[ibada]] na [[karama]] (1Kor 11:20-33; 12:4-13:13; 14:18-40), na hatimaye [[ufufuko]] wa wafu (1Kor 15:1-28,33-49).
 
Mwishoni kuna maagizo, [[taarifa]] na salamu mbalimbali (1Kor 16:1-4).
 
Ndiyo sababu barua ni ndefu na inagusa mambo mengi ambayo Paulo aliyatazama kwa [[hekima]] ya juu inayotokana na [[msalaba]] wa [[Kristo]].
 
==Madondoo muhimu==
Kati ya mambo mengi muhimu, barua hiyo inatunza simulizi la kwanza la [[karamu ya mwisho]] ya [[Bwana]] [[Yesu]] (11:23-25) na [[kanuni ya imani]] ya kwanza inayoorodhesha pia matokeo ya [[Yesu Kristo]] Mfufuka (15:3-8).
 
== Marejeo ==
Mstari 39:
* [http://www.intratext.com/IXT/SWA0013/_INDEX.HTM] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
 
===VinginevyoVingine===
{{wikisource|1 Corinthians}}
{{wikiquote}}