Tofauti kati ya marekesbisho "Waraka kwa Wakolosai"

76 bytes added ,  mwaka 1 uliopita
no edit summary
 
{{Agano Jipya}}
[[File:Harleianus 5557 (first page of Colossians).jpg|thumb|right|220px|[[Ukurasa]] wa kwanza wa [[waraka]] huu katika [[gombo]] [[Minuscule 321]].]]
'''Waraka kwa [[Wakolosai]]''' ni kati ya [[vitabu]] 27 vya [[Agano Jipya]] ambalo pamoja na [[Agano la Kale]] linaunda [[Biblia]] ya [[Wakristo]].
 
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya [[maendeleo]] ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
== Muda wa uandishi ==
[[Barua]] hiyo ni mojawapo kati ya zile za mwishomwisho za [[Mtume Paulo]] na inaonyesha maendeleo ya [[teolojia]] yake, hasa kutokana na [[muda]] mrefu wa kutafakari aliojaliwa kifungoni.
 
== Mazingira ==
[[Kanisa]] la [[Kolosai]], [[mji]] wa [[biashara]] karibu na [[Efeso]] lilianzishwa na [[mwanafunzi]] wa Paulo, labda [[Epafra]], halafu likaingiwa na mafundisho ya ajabuajabu yaliyochanganya mambo ya [[Kiyahudi]] na ya [[Upagani|Kipagani]] na yaliyozingatia mno ukuu wa [[malaika]] juu ya [[ulimwengu]].
 
Ndiyo sababu huenda Paulo, akiwa kifungoni [[Roma]] kati ya miaka [[61]] na [[63]], akawajibika kuliandikia barua inayoonyesha kuwa [[Yesu Kristo]] ni mkuu kuliko wote: vyote kabisa viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake, tena katika [[ubinadamu]] wake umo utimilifu wote wa [[Mungu]].
 
Yeye ndiye “[[fumbo]]” kwa kuwa Mungu ametimiza mpango wa [[wokovu]] kwa njia yake.
 
Hakuna sababu ya kutafuta kwingine [[hekima]] na [[maarifa]], wala ya kujiwekea masharti ya kibinadamu yasiyosaidia kuokoka (Kol 1:13-29; 2:6-3:4; 3:5-17).
 
== Mpangilio ==
Mpangilio wa barua ni kama kawaida ya barua za Paulo: utangulizi, mafundisho ya [[imani]], maonyo kuhusu [[uzushi]], [[mawaidha]] na hatima.
 
==Marejeo==
 
== Viungo vya nje ==
{{wikisource|Colossians (Bible)|Colossians}}
===Tafsiri ya Kiswahili===
{{wikiquote}}=
 
===Tafsiri ya Kiswahili===
* [http://www.intratext.com/IXT/SWA0013/_INDEX.HTM] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
 
===VinginevyoVingine===
{{wikisource|Colossians (Bible)|Colossians}}
{{wikiquote}}
* [http://www.gospelhall.org/bible/bible.php?passage=Colossians+1 ''Online Bible'' at GospelHall.org]
* [http://www.earlychristianwritings.com/colossians.html Collection of translations and commentary on Colossians]
[[Jamii:Vitabu vya Agano Jipya|Kol]]
[[Jamii:Mtume Paulo]]
[[Jamii:Kolosai]]