Waraka kwa Waebrania : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
'''Barua kwa Waebrania''' ni kati ya [[vitabu]] 27 vya [[Agano Jipya]] katika [[Biblia ya Kikristo]].
 
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya [[maendeleo]] ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
== Mazingira ==
[[Miaka ya 60]] [[B.K.]] [[Mkristo]] mwenye [[asili]] ya [[Kiyahudi]] na [[elimu]] ya [[Kiyunani]], aliwaandikia [[Wakristo wa Kiyahudi]] wenzake si [[barua]] hasa, bali [[hotuba]] kamili iliyoambatanishwa na kipande cha barua.
 
Hali iliyosababisha [[uandishi]] ni baadhi yao kuvutiwa tena na [[dini]] yao asili na [[ibada]] zake [[Hekalu la Yerusalemu|hekaluni]]: [[kishawishi]] kilikuwa kikubwa hasa kwa sababu [[Kanisa]] lilikuwa bado mwanzoni, bila [[Maabadi|mahali maalumu pa kusali]] wala ibada za [[fahari]].
 
[[Mwandishi]] aliwaonya kuwa wakimuasi [[Yesu]] hawamrudii [[Mungu]] aliye hai, aliyejifunua hasa katika [[Mwana wa Mungu|Mwanae]], bali [[Msalaba wa Yesu|wanamsulubisha]] tena kwa makusudi mazima na kustahili tu [[moto wa milele]].
Mstari 13:
== Mada ==
[[File:Storia dell' Antico e Nuovo Testamento - 10 - Sommo Sacerdote.jpg|thumb|right|[[Kuhani Mkuu]] wa Agano la Kale alivyochorwa mwaka [[1821]].]]
Sehemu kubwa ya [[maandishi]] hayo inalinganisha [[Yesu Kristo]] na [[ukuhani]] wake katika [[hekalu]] la [[mbinguni]] upande mmoja, na ukuhani wa [[Agano la Kale]] huko [[Yerusalemu]] upande mwingine.
 
Hivyo mwandishi alielekeza [[safari ya kiroho]] katika [[imani]] inayofanana na ile ya [[watakatifu]] wa Agano la Kale.
Mstari 20:
 
== Ubora wa kitabu hiki ==
[[Ubora]] wake ni kulinganisha mambo ya kale na utimilifu wake katika [[Agano Jipya]], pia kuthibitisha ukuu wa [[Kristo]] kama kuhani wa [[milele]] (Eb 1:1-2:4; 4:11-5:10; 7:1-8:13; 10:19-11:40; 13:22-25). Hiyo inaendana na [[ufasaha]] wa [[lugha]].
 
== Marejeo ==
Mstari 52:
 
[[Jamii:Vitabu vya Agano Jipya|Ebr]]
[[Jamii:Uyahudi]]