Mahema madogo yanatumiwa pia kama kinga ya muda kwa [[burudani]] kama camping au [[matembezi]] marefu. Mahema makubwa zaidi hutumiwa na [[jeshi]] kwa kambi za muda, pia wakati wa [[maafa]] kama watu hawana [[nyumba]] tena: kwa mfano baada ya [[tetemeko la ardhi]] au [[mafuriko]]. Mahema makubwa sana zatumiwa kwa mikutano mahali pasipo [[ukumbi]] mkubwa kiasi cha kutosha.
Katika ukulima wa kisasa hema pia hutumika kukuzia mimea kama vile katika ukuzanjiukuzaji wa mime bila mchanga unao julikana kwa Kingereza kama ''Hydroponic.''<ref>{{Cite web|url=https://www.maximumyield.com/definition/4571/grow-tent|title=What is Grow Tent? - Definition from Maxyield|language=en|work=www.maximumyield.com|accessdate=2019-07-02}}</ref> Hema hizi maarufu kama ''Grow Tents'' zina miundo na ukubwa tofauti na hukinga mimea kutokana na athari za hali ya anga, wadudu na wanyama waharibifu au kukuziwa mimea inayohitaji kuangaliwakutunzwa kwa makini<ref>{{Cite web|url=http://gardenclub.homedepot.com/reasons-use-grow-tent/|title=7 Reasons to Use a Grow Tent|date=2017-12-12|language=en-US|work=The Home Depot Garden Club|accessdate=2019-07-02}}</ref>. Hema za kukuzia mimea ni maarufu sana na wakulima wa miche na wakulima wa [[mbangi]].<ref>{{Cite web|url=http://growtentexperts.com/|title=Grow Tent Experts: Weed Grow Tent Reviews & Buying Guide 2018|language=en-US|work=Grow Tent Experts|accessdate=2019-07-02}}</ref>