Sungusungu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Kipala alihamisha ukurasa wa Sungusungu hadi Sungusungu (sisimizi): Matumizi ya kawaida Tanzania ya neno ni kutaja walinzi wa jadi wa kibinadamu
Tag: New redirect
 
Removed redirect to Sungusungu (sisimizi)
Tag: Removed redirect
Mstari 1:
#REDIRECT<sup>Kuhusu sisimizi tazama [[Sungusungu (sisimizi)]]</sup>
 
'''Sungusungu''' ni namna ya kutaja walinzi wa jadi nchini Tanzania.
Jina la Sungusungu pamoja asili ya vikundi vyao lilitokea katika jamii za [[Wasukuma]] katika [[Tanzania|Tanzania ya Magharibi]].
 
Jina hili lilianza kupata umaarufu tangu miaka ya 1980 kati ya Wasukuma<ref>Leticia K. Nkonya, Rural Water Management in Africa: The Impact of Customary Institutions in Tanzania,Cambria Press 2008, ISBN-10: 1604975377, ISBN-13: 978-1604975376, uk. 128, [https://books.google.co.tz/books?id=QaoHg7HiikwC&pg=PA130&dq=sungusungu&hl=en&sa=X&ved=0ahUKEwjRtsqru6PjAhUDJVAKHQgsDa4QuwUIKjAA#v=onepage&q=sungusungu&f=false online hapa]</ref> walioona matatizo ya wizi wa mifugo na ujambazi kwenye barabara baada ya vita ya Uganda na kurudi kwa wanajeshi wengi Tanzania.
 
Kufuatana nakumbukumbu ya wenyeji, walianzia wilayani Kahama Kata ya Janna na baadaye kuzinduliwa rasmi Kata ya [[Mwalugulu|Mwaluguru]], mwaka 1982<ref>[https://mobile.mwananchi.co.tz/Habari/Shindikilagi-ya-Sungusungu-ilivyotumika--kwa-mauaji-/1597580-2127320-format-xhtml-oylu2w/index.html Shindikilagi ya Sungusungu ilivyotumika kwa mauaji ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’], taarifa ya Shija Felician, kwenye gazeti la Mwananchi, 28/12/2013</ref>. Baada ya kuona polisi haikuadhibu wezi wa mifugo na kujisikia viongozi kadhaa upande wa serikali walishirikiana nao, wananchi wa Janna waliunda kundi la vijana waliomchagua chifu kati yao na kuwinda wezi. Harakati hii ilienea kwenye kata za jirani. Wezi na majambazi waliuawa mara nyingi lakini vijijini Wasungusungu waliendelea kuwaua pia watu walioshtakiwa kuwa Wachawi. Baada ya polisi kuwatafuta viongozi na kuwakamata Wasungusungu walipata kibali cha rais Julius Nyerere waweze kuendelea<ref>Hervé Maupeu & Kimani Njogu, Songs and Politics in Eastern Africa, Mkuki Na Nyota Publishers 2007, ISBN-10: 9987449425, ISBN-13: 978-9987449422, [http://www.africanbookscollective.com/books/songs-and-politics-in-eastern-africa/Songs%20and%20Politics%20in%20Eastern%20Africa%20-%20Foreword.pdf online hapa]</ref>.
 
Kati ya Wasukuma kulikuwa na utaratibu wa Wasungusungu; walisimamiwa na "ntemi" wao aliyesaidiwa na makamu wake, "ntwale" na katibu. Chini yao yuko "Kamanda" anayeongoza vijana wanoenda kuwakamata wezi au washtakiwa. Wote walishauriana katika "bunge la Sungusungu".
 
Kutoka Usukuma mtindo wa sungusungu uliendelea kusambaa kama chombo cha usalama kwa kusaidiwa na vyombo vya dola hadi kuenea juu ya asilimia 20 za Watanzania wote.<ref>Joseph F Donnermeyer, The Routledge International Handbook of Rural Criminology, 2016, uk. 411, ISBN-13: 978-1138799745, ISBN-10: 1138799742 [https://books.google.co.tz/books?id=ED4SDAAAQBAJ&pg=PA412&dq=sungusungu&hl=en&sa=X&ved=0ahUKEwjRtsqru6PjAhUDJVAKHQgsDa4QuwUINDAC#v=onepage&q=sungusungu&f=false online hapa]</ref>
 
Katika miaka ya baadaye mitindo ya ulinzi wa wakazi wa eneo wasio watumishiwa serikali lakini wanashirikiana na vyombo vya serikali imesambaa pia katika miji ya Tanzania<ref>https://www.ippmedia.com/sw/safu/tuimarishe-usalama-kwa-maboresho-ya-sungusungu</ref>.
 
==Marejeo==
<references/>
 
[[jamii:Serikali]]