Mfuko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
restore less spammy
No edit summary
Mstari 9:
 
Ingawa karatasi ilikuwa imetumika kwa ajili ya kufunika kwenye [[China]] ya kale tangu [[karne ya 2 KK]], matumizi ya kwanza ya mifuko ya karatasi (kwa ajili ya kuhifadhi [[ladha]] ya [[chai]]) nchini China ilikuja wakati wa [[nasaba]] ya baadaye iliyokuwa imara.
 
== Mfuko wa kubebea kwa mkono ==
Mfuko wa kubebea kwa [[mkono]] (kwa Kiingereza "handbag") hubebwa na [[wasichana]] na [[wanawake]] kwa jumla wanapotembea. Mfuko huu huwawezesha kubeba vitu vidogovidogo kama [[vipodozi]], kiio cha mkono, [[viatu]] badala na [[nguo]]. Mfuko huu huwa mdogo na kwa hiyo, hauwezi ukawekwa vitu vingi. Kwa kubebewa mkononi, mbebaji pia hataweza kubeba vitu vizito.
 
== Mfuko wa mtoto ==
Mfuko huu ambao pia huitwa mfuko wa nepi (baby bag au nappy bag) hutumiwa kubebea nepi za mtoto. Wamama waliojaliwa watoto hubebea pia maziwa ya watoto wao wachanga, nguo badala za mtoto pamoja na mashuka ya kubebea mtoto mama anapoenda safari na mtoto wake.
 
== Mfuko wa kubebea mzigo ==
Mfuko huo (backpack) hutumiwa na wanafunzi wa shule kwa kubebea vitabu. Pia huonekana kwa watu walio kwa ziara huku wamebeba mizigo yao kwa nyuma.
 
Mfuko huu huwa ni mzuri kuliko ule wa kubebea kwa mkono maana huwezesha mbebaji kubeba mizigo mingi zaidi. Mfuko huo waweza kubebea hadi kilo kumi haswa kwa watu wanaoenda ziara za mbali au kwa wakwea milima.
 
Kwa mizigo ambayo ni mingi zaidi, msafiri anaweza kutumia "travel suitcase" ambayo ni kubwa, yaweza kubeba uzito mwingi na pia ina vigurudumu ili usichoke kwa kubeba kwani waweza kuvivuta haswa kwa barabara za lami.
 
{{mbegu-utamaduni}}