Mke wa Kurusi (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 11:
 
==Jina==
Mke wa Kurusi ilijulikanalilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi na mabaharia Waswahili walioitumia kupata njia baharini wakati wa usiku.<ref>ling. Knappert 1993</ref>
Jina la Mke wa Kurusi lina sehemu mbili; “mke” ni kifupi cha mwanamke na “kurusi” linamaanisha “kiti” kutokana na jina la Kiarabu كرسي kursi. Jina lote ni tafsiri ya Kiarabu ذات الكرسي ''dhat al-kursi'' yani “Bibi wa kiti” ambayo tena ni tafsiri tu ya Kilatini “mulier sedis” yenye maana hiyihiyo. Yote inarejelea mitholojia ya [[Ugiriki ya Kale]] iliyoona hapa picha ya malkia maridadi Cassiopeia akikalia kiti chake cha kifalme. Cassiopeia alikuwa mke wa mfalme Kifausi (Cepheus) akajivunia kuwa yeye mwenyewe na binti yake Mara (Andromeda) ni wazuri kushinda mabinti wa Poseidon mungu wa bahari. Hapo Poseidon aliamua kumwadhibu kwa kutuma dubwana Kestusi dhidi yake. Cassiopeia pamoja na mumewe mfalme Kifausi waliamua kumtua binti Mara-(Andromeda) kama sadaka kwa Ketusi kwa kumfunga kwenye ufuko wa bahari ili aliwe na dubwana huyu lakini shujaa Farisi (Perseus) akaingia kati na kumwokoa. Baadaye wote waliinuliwa angani kama nyota <ref>ling. Allen, Star-Names and their Meanings uk, 117</ref> kwa hiyo tunaona Mke wa Kurusi (Cassiopeia) jirani na makundinyota ya Kifausi na Mara, halafu Ketusi na Farisi aliyekuja kumwokoa Mara katika simulizi ya mitholojia..