Sabato : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
No edit summary |
d Masahihisho aliyefanya Frank de dfl (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Magioladitis Tag: Rollback |
||
Mstari 17:
[[Tabia]] ya pekee ya amri hii ni [[sharti]] la kuwapa hata [[wafanyakazi]] na [[watumwa]] nafasi hii ya kupumzika, hasa inavyotajwa katika [[Kumbukumbu la Torati]] 5:12-15 ambamo sababu si [[uumbaji]] bali [[ukombozi]] ambao Mungu kwa njia ya Musa aliwatoa Waisraeli utumwani [[Misri]]. Hivyo amri hii inatazamwa kama [[sheria]] ya kwanza ya kutunza [[haki za wafanyakazi]].
Kadiri ya Kutoka 31:13-17 adhimisho la Sabato lilitolewa na Mungu kwa Waisraeli kama [[ishara]] ya [[agano]] la kudumu kati yake na wao
== Mapokeo ya Talmudi ==
Mstari 28:
[[Wayahudi huria]] hawachukui amri hizi vikali vile. Kwa mfano Myahudi huria asingeandika chochote kinachohusika na kazi yake lakini hana shida kuandika [[barua]] isiyo ya kikazi. Atajaribu kuepukana na tendo la kununua kitu [[duka]]ni lakini kama kuna haja atafanya hivyo.
Wayahudi wote wafundisha ya kwamba sheria zote za Sabato zaweza kuvunjwa kama [[uhai]] wa [[binadamu]] uko hatarini.
== Wakristo na Sabato ==
Katika [[Ukristo]] Sabato imehamishwa
Chanzo cha badiliko hilo kinaonekana katika taarifa ya [[Matendo ya Mitume]] 20:7 inayoonyesha ya kwamba wakati wa [[Mtume Paulo]] Wakristo walikutana siku ya kwanza ya juma. Sababu yake ilikuwa kukumbuka [[ufufuko wa Yesu]] aliyetoka [[kaburi]]ni siku hii ya kwanza yaani Jumapili
Agano Jipya halielezi badiliko hili lilitokeaje, lakini linahusianishwa na matukio mawili ya Kanisa katika [[karne ya 1]]: polepole Wakristo wa mataifa waliwapita wale wa Kiyahudi kwa idadi na bidii, nao hawakujali tena mambo mbalimbali ya [[Agano la Kale]]; amani kati ya Wakristo na Wayahudi ilizidi kupungua, na baada ya maangamizi ya [[Hekalu la Yerusalemu]] ([[70]] [[BK]]) hao wa mwisho waliwakataza hao wa kwanza wasiendelee kushiriki ibada zao sinagogini. [[Barua kwa Wakolosai]] 2:16 inawahimiza Wakristo hao wasijisikie kubanwa na masharti ya Kiyahudi wala kusumbuliwa na mtu kuhusu Sabato na siku nyingine za [[kalenda ya Kiyahudi]].
|