Majadiliano ya Wikipedia:Mradi wa Tanzania : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
→‎UTAMADUNI: mjadala mpya
Mstari 10:
 
:Je kata yako ni [[Mwembe (Same)]]? Mpendwa hapa tuko kwenye intaneti, na tovuti hii ni kamusi. Tunakusanya habari ili habari hizi zipatikane rahisi kwa watu wengi. Kwa watu kijijini njia ya kuboresha hali ni kuongea nao na kupanga pamoja na kufanya. Inaneti haiwasaidii moja kwa moja. Kile kinachowezekana hapo: ukiwa na habari kuhusu kata yako uongeze habari hizi katika makala ya [[Mwembe (Same)]]. Kabla ya kufanya hii ujiandikishe na kufungua akaunti inarahisisha mawasiliano tukijua tunaongea na nani. Wasalaam. '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 09:06, 20 Septemba 2015 (UTC)
 
== UTAMADUNI ==
 
Utamaduni wa Watu wa Kata ya Tawa (Waluguru) ni aina iliyo tofauti kabisa na makabila mengine. Mkuu wa Kata hiyo kihistoria (Kama ilivyokuwa kwa Kata za Kibogwa, Kibungo Juu, Tegetero, Kisemu, Konde, Kasanga, na baadhi ya Maeneo yote ya Mgeta) alijulikana kwa jina maarufu la Kingalu. Aidha, miongoni mwa maeneo maarufu ya Kitamaduni ni pamoja na Maporomoko ya Mto Mmanga. Wenyeji wa Morogoro huwarithisha vizazi vyao maadili, mila, tamaduni na desturi vizazi vyao kwa unyago na ngoma mbalimbali.
 
Ni utamaduni wa wenyeji wa Kata hiyo, pale ambapo binti amevunja uongo anawekwa ndani kwa muda usiopungua mwezi mmoja ambako anakula na kulala tu bila kufanya kazi yoyote na wala bila kuonana na mtu yeyote yule isipokuwa ni kwa yule aliyeteuliwa na ukoo kuonana naye. Akiwa ndani binti hupewa mafundisho ya aina mbalimbali, hufundishwa juu ya kuanzisha na kukuza familia, mahusiano kati ya mume na mke, maadili, nidhamu, mila, desturi na utamaduni katika jamii. Aidha, siku ya mwisho ya binti kutoka kukaa ndani, kabla ya kutoka nje inaandaliwa sherehe kubwa ambapo vyakula na vinywaji mbalimbali huandaliwa, ngoma mbalimbali huchezwa kwa siku mbili (inategemea matakwa ya familia). Kwa vijana wa kiume historia inaonesha kuwa walikuwa wakipewa mafundisho (yanayoshabihiana na mafundisho ya mabinti) wakati wa kuingizwa jando (kipindi cha kutahiriwa).
 
Utamaduni wa ngoma za wenyeji wa Kata ya Tawa umechanganyika na wa ngoma za asili ya makabila za Kizaramo, Kipogoro na Wamakonde. Ngoma maarufu kwa wenyeji wa Kata ya Tawa ni; Mganda, Kibende, Mbeta, Gombesugu, Mkwajungoma n.k.)
Return to the project page "Mradi wa Tanzania".