Tofauti kati ya marekesbisho "Wapangwa"

107 bytes added ,  mwaka 1 uliopita
no edit summary
 
'''Wapangwa''' ni [[kabila]] la [[watu]] kutoka [[Milima Livingstone]] karibu na [[pwani]] ya [[mashariki]] ya [[Ziwa Nyasa]], [[wilaya ya Ludewa]], [[Mkoa wa Njombe]], [[kusini]] mwa nchi ya [[Tanzania]]. [[Mwaka]] [[2002]] [[idadi]] ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.
 
[[Mwaka]] [[2002]] [[idadi]] ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.
 
[[Lugha]] yao ni [[Kipangwa]].
 
==Historia==
Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya [[Ludewa]] (Madunda, Mawengi, Mlangali, Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea [[Njombe]]. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni [[vita]], maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile [[Malawi]] na [[Msumbiji]], kwa ajili ya vita.
 
==Uchumi==
Wapangwa hulima [[mazao]] mbalimbali ya [[chakula]] katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya [[mito]]. Hulima kwa [[ushirika]] unaoitwa njhiika. Pia hulima mazao ya [[biashara]] kama [[kahawa]], [[chai]], [[pareto]], [[mahindi]]. Kabila hili pia hupata [[matunda]] ya asili kama vile: masada, savula, makuhu, mahofita, mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.
 
Pia ni [[wafugaji]] wa [[makundi]] madogomadogo ya [[ng'ombe]], [[mbuzi]], [[kondoo]] na [[nguruwe]] ([[kitimoto]]). Tena Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na [[uwindaji]] wa [[wanyamapori]] kama vile (kwa lugha yao) nyhaluchi ,mahtu ngwehe, sudi, ng'ese, ng'wali ni videke.
 
==Utamaduni==
Chakula chao ni [[ugali]] wa [[mahindi]], [[ulezi]] na [[mtama]] kidogo. [[Kitoweo]] cha vyakula hivyo ni [[maharage]], [[samaki]], [[nyama]] na jamii ya [[Mboga|mbogamboga]].
 
[[Kinywaji]] chao ni [[pombe]] (ukhimbi) yaani kangala, komoni, [[ulanzi]] ambao hugemwa kutoka katika [[mmea]] uitwao [[mlanzi]]. Ulanzi ni pombe ya asili sana kwa Wapangwa, maana ni [[jadi]] kwao kunywa ulanzi, na hata [[watoto]] wadogo hupewa ulanzi kama [[juisi]]. Ulanzi, kwa Wapangwa ni pombe ambayo inaheshimika sana, maana hata wanapokwenda [[Shamba|shambani]], huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka [[mfanyakazi]] shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya [[kazi]], mpaka apewe ulanzi.
 
Hata katika [[harusi]] na [[sherehe]] nyingine za kimila kama vile kujengea [[Kaburi|makaburi]] (Mahoka), [[mila]] za kumrudisha [[mjane]] nyumbani (Ngotora), mila za kuabudu [[miungu]], n.k., ulanzi ndio huwa unatumika zaidi ya pombe nyingine.
 
Kwa hiyo, Wapangwa wote (kama vile kina Willah, Haule, Muligo, Mtweve, Ngairo, Mwinuka n.k.), ambao bado wanatii mila na [[desturi]] zao, ulanzi kwao ni jadi.
Usafiri wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.
 
[[Mavazi]] yao ya asili ni [[nguo]] zilizotengenezwa kwa [[ngozi]] za [[wanyama]] pamoja na magome ya [[miti]] ya misambi ambayo hupondwapondwa, hufumwa na kupakwa mono.
[[Nyumba]] zao kwa sasa ni za [[matofali]] ya [[udongo]] ya kuchoma na kuezekwa kwa [[bati]], hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti kugandikwa kwa [[udongo wa mfinyanzi]] na kuezekwa kwa [[nyasi]] aina ya hunji na lihanu.
 
[[Usafiri]] wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.
== Viungo vya Nje ==
 
[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]
== Viungo vya Njenje ==
* [http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]
 
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{Makabila ya Tanzania}}
[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Wilaya ya Ludewa]]