Shaka Zulu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:KingShaka.jpeg|thumb|right|Picha ya Shaka Zulu mnamo mwaka 1824]]
'''Shaka''' (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: '''Shaka Zulu''', Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 [[BK]]) alikuwa kiongozi wa [[Zulu|Wazulu]] aliyebadilisha ukoo mdogo wa Wanguni[[Nguni|Kinguni]] kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala sehemu kubwa za [[Afrika Kusini]] kati ya mito ya [[Phonogolo]] en [[Mzimkhulu]].
 
Sifa zake ni kutokana uwezo wake wa kupanusha utawala wake kutoka eneo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi, jinsi ilivyo na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi, zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka ilianzisha kipindi cha [[mfecane]] yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya Afrika Kusini .
 
==Maisha yake==
 
===Kijana===
Shaka alikuwa mtoto wa chifu [[Senzangakhona ka Jama]] na [[Nandi]] binti wa chifu wa [[Langeni]]. Jina lake ni kutokana na neno la kizulu "iShaka" linalomtaja mdudu ambaye katika iamni ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya wakinamama. Jina hili ni dalili la kuzaliwa nje ya utaratibu. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba aneyejulikana rasmi akisikia udharau ya watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.
 
Kama kijana Shaka alikaa kwa kabila kubwa zaidi ya [[Mthethwa]] alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa Wazulu walikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthehthwa alikuwa [[Dingiswayo]] alieyeanzisha utaratibu mpya wa [[impi]] yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha baadaye.
 
===Kurudi kwa Wazulu===
Baada ya kifo cha babake Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi maadui wa utoto wake akiwaua kwa njia mbalimbali.
 
Shaka aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi huyu aliuawa vitani na kabila la [[Ndwandwe]] mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na koo au makabila madogo jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui wasiouawa lakini waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.
 
==Kupanusha utawala wake==
Baada ya kifo cha Dingiswayo mw. 1817 Shaka alishambulia kabila kubwa la Ndwandwe akawashinda kwenye mapigano ya kilima cha Gqokli kwa sababu ya mbinu zake za kijeshi ingawa idadi ya watu wake ilikuwa nusu tu ya adui.
 
Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundu vya jirani na kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi vya kijeshi vya Shaka.
 
Alituma viongozi au majenerali zake pamoja na impi pande mbalimbali hadi Msumbiji au pia Zimbabwe. Vita hizi zilisababisha makabila mengine kuhamahama wakishambulia majirani yao au vikundi vingine kuungana ili wawe na uewezo wa kushindana na Wazulu. Vikundi kama Ndebele huko Zimbabwe au hata Wangoni katika Tanzania ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
 
===Kifo===
Utawala wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizomletea maadui wengi. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na huzuni kiasi cha kuua watu 7000 kati ya wanajeshi wake na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua na kutupa maiti shimoni.
 
Dingane alimfuata Shaka akaua vingozi wengi waliokuwa waaminifu kwa Shaka.
 
 
==Mafanikio ya kijeshi ya Shaka==
Shaka aliboresha utaratibu alioukuta katika utumishi wa Dingiswayo. Kati ya mambo mapya aliyoanzisha ni yafuatayo:
 
===Silaha mpya===
Utamaduni wa Wanguni ulikuwa mikuki ya assegai na kila mtu alibeba tatu. Shaka aliona silaha za kutupwa ni hasara. Aliongea mwenyewe na wahunzi akaanzisha silaha katikati ya mkuki na upanga - "Iklwa". Haikufaa kutupwa bali kushikwa hivyo kuwalazimisha watu wake kushambulia na kuwa karibu na adui. Aliwapatia pia vigao vizito vya ngozi ya ngòmbe.
 
===Kutembea bila viatu===
Alilazimisha watu wake kuacha vyandalua na viatu na kutembea pekupeku. Hii iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao. Inasemekana ya kwamba Shaka aliua wote waliolalamika walipoamuru kuacha viatu vyao.
 
===Kuwa na vikosi vya kusaidia mizigo===
Shaka alitumia wavulana wadogo kuanzia umri wa miaka sita waliongozana na impi wakibeba mizigo au kuwafuata wanajeshi kwa ngombe kama chakula. Hata hii iliharakisha mwendo wa impi zake.
 
===Impi za hirima===
Hirima au vikundi vya kujumuisha watu wa umri moja ni tabia ya utamaduni kwa Wabantu wengi. Shaka alipoanzisha impi zake -badala ya kushambulia na watu wake wote mara moja jinsi ilivyokuwa kawaida awali- alitumia vikundi vilivyokuwepo tayari kiutamaduni kama msingi wa impi zake.
 
===Muundo wa Kichwa cha Mbogo===
Shaka alianzisha mpagilio wa impi zae vitani kwa umbo la "Kichwa cha Mbogo":
1. vikosi viwili upande wa kushoto na kulia vilikuwa kama "pembe za mbogo"
2. kikosi kikubwa cha katikati kilikuwa kama "uso" au "kifua"
3. vikosi vya ziada au vya wazee vilikuwa "viuno" vilivyotumika ama kuongeza uzito wa mashambulio panapohitajika au kuimarisha utetezi pale ambako adui alisogea mbele.
 
{{mbegu}}
 
[[Category:Afrika Kusini]]