Tofauti kati ya marekesbisho "Uingereza"

No change in size ,  miaka 2 iliyopita
no edit summary
== Jiografia ==
[[Picha:Widecombe in the Moor, Devon.jpg|thumb|Mazingira ya vilima vya Devon, kusini-magharibi ya Uingereza]]
Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambayoambacho nindicho kisiwa kikubwa cha [[Ulaya]]. Inapakana na [[Welisi]] upande wa magharibi na [[Uskoti]] upande wa kaskazini.
 
Upande wa magharibi iko Bahari ya Eire, na ng'ambo yake kisiwa cha [[Eire]] (Ireland). Upande wa mashariki iko [[Bahari ya Kaskazini]], ng'ambo yake [[Denmark]], [[Ujerumani]] na [[Uholanzi]]; upande wa kusini ikouko [[Mfereji wa Kiingereza]] halafu kwenye kusini-magharibi [[Bahari Atlantiki]], ng'ambo yake [[Ufaransa]] na [[Ubelgiji]]. Tangu mwaka [[1994]] chini ya mfereji huo kuna njia ya reli kwa [[tobwe]] chini ya mfereji inayounganisha Uingereza na Ufaransa.
 
Eneo la Uingereza ni takriban [[km²]] 130,000 na hivyo theluthi mbili za kisiwa cha Britania.
 
Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni [[Isle of Wight]] katika kusini. Pwani zake ni ndefu, hakuna mahali palipo mbali zaidi ya km 113 kutoka [[bahari]].
 
Sehemu kubwa ya nchi ni ama tambarare au vilima vidogo; mwinuko wa juu ni Scafell Pike yenye kimo cha mita 978. Milima mirefu ya Britania iko katika Welisi na Uskoti.
===Tabianchi===
Tabianchi ya Uingereza inaathiriwa na mahali pake baharini inayopitiwa na [[Mkondo wa Ghuba]] na [[latitudo|latitudo ya kaskazini]]. Athari hizi zinaleta tabianchi fufutende ya kibahari; kwa wastani baridi haishuki chini ya 0 [[°C]] na joto halipandi juu ya 32 °C. Hata hivyo vipindi vya [[jeledi]] au joto kali zaidi vinaweza kutokea kwa siku kadhaa. Miezi ya baridi ni Januari na Februari. Julai kwa kawaida ni mwezi mwenyo joto zaidi. Hali ya hewa mara nyingi ni nyevunyevu na mvua inaweza kutokea mwaka wote. Vipindi vya mvua na jua hubadilishana haraka.
 
 
===Miji ya Uingereza===
Mji Mkuu ni [[London]]. Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: [[London]] (wakazi 9,787,426), [[Manchester]] (2,553,379), [[Birmingham]] (pamoja na West Midlands 2,440,986), [[Leeds]] (pamoja na West Yorkshire 1,777,934), [[Sheffield]], [[Bradford]] na [[Liverpool]].
 
 
=== Mito ya Uingereza ===
[[Picha:CanalettoSomersetHouseTerrace.jpg|thumb|left|320px|Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750]]
Kutokana na tabianchi yenye mvua ya kutosha kuna mito mingi nchini. Mito mirefu ni Thames (km 346) na Severn (km 350).
 
* [[Severn (mto)|Severn]] (mto mrefu wa [[Britania]])
* [[Thames (mto)|Thames]] (mto mrefu katika Uingereza)