Ubaridi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|300px|Siwa barafu ambalo kikawaida husababishwa na baridi.'''Ubaridi''' ni uwepo wa hali ya chini ya halijot...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:33, 8 Septemba 2019

Ubaridi ni uwepo wa hali ya chini ya halijoto katika kitu fulani au eneo fulani, lakini hasa katika angahewa.Katika hali ya kawaida baridi huwa ni hali ya mtazamo binafsi.Mpaka wa chini kabisa wa baridi ni sifuri halisi ambayo katika skeli ya Kelvin husomwa kama 0.00K.

Siwa barafu ambalo kikawaida husababishwa na baridi.

Kwakuwa halijoto huhusisha nishatijoto inayoshikiliwa na kitu au sampuli ya maada, amabayo ndiyo nishatimwendo ya chembe ziundazo maada, kitu kitakuwa na nishatijoto ndogo pale kinapokuwa cha baridi na nishatijoto kubwa pale kinapokuwa cha moto. Kama kungalikuwa na uwezekano wa kuupooza mfumo fulani mpaka halijoto ya sifuri halisi, mwendo wote wa chembe katika sampuli ya maada ungekoma and chembe hizo zingekuwa tuli katika mtazamo huu wa kisasa. Kitu hicho kingechukuliwa kuwa na nishatijoto ya sifuri.