Kiini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 13:32, 8 Septemba 2019

Kiini ni eneo dogo la kiatomiki, lililosongamana lenye kuundwa na protoni na neutroni lililo katikati ya atomi,eneo hili liligunduliwa mnamo mwaka 1911 na mwanasayansi Ernest Rutherford kwa kutegemea jaribio la folili ya dhahabu lililofanywa mwaka 1909 na mwanasayansi Geiger–Marsden. Baada yaugunduzi wa neutroni katika mwaka 1932,modeli za kiini zilizokuwa zikijumuisha protoni na neutroni ziliundwa kwa haraka na Dmitri Ivanenko pamoja na Werner Heisenberg. Atomi inaundwa na kiini kilicho na chaji chanya,pamoja na wingu la elektroni lenye chaji hasi linaloizunguka, vyote vikishikiliwa na nguvu ya umeme-tuli.Karibu uzito wote wa atomi unapatikana katika kiini, ukichangiwa na asilimia chache za wingu la elektroni. Protoni na neutroni zinafungamanishwa pamoja kuunda kiini kwa nguvu ya nyuklia.

Modeli ya kiini cha atomi ikikionesha kama fungo gumu la aina mbili za chembekiini yaani protoni(nyekundu) na neutroni(samawati).Katika mchoro huu, protoni na neutroni zinaonekana kama vipira vidogo vilivyoshikamana pamoja.