Ramses II : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|250px|[[Sanamu yake huko Abu Simbel.]] thumb|190px|Ramses II akiwa [[mtoto (Cairo Muse...'
 
No edit summary
Mstari 3:
[[File:The great Sesostris (Rameses II) in the Battle of Khadesh.jpg|right|thumb|241x241px|Ramses II katika [[mapigano ya Khadesh]].]]
[[File:Kadesh.jpg|thumb|left|[[Kigae]] cha [[amani]] na [[Hattusili III]] wa [[Hittites|Hatti]], [[Istanbul Archaeology Museum]].]]
'''Ramses II''' au '''Rameses Mkuu''' au '''Sese''' ([[1303 KK|1303]] hivi - Julai au Agosti [[1213 KK]])<ref>{{cite encyclopedia |year=2004 |title=Ramses |encyclopedia=Webster's New World College Dictionary |publisher=Wiley Publishing |location= |url=http://www.yourdictionary.com/Ramses}}</ref> alikuwa [[Farao]] wa [[Misri]] miaka [[1279 KK|1279]]–[[1213 KK]], wa tatu katika [[Nasaba ya 19]] ya [[Misri ya Kale]].
 
Mara nyingi anasifiwa kama Farao bora. Waandamizi wake na Wamisri wa baadaye walimuita "Mzee Mkuu".
Mstari 10:
 
Tena alishughulikia sana [[ujenzi]] wa [[Mji|miji]] n.k. Pia kwa sababu hiyo, wengi wanaona ndiye Farao aliyepambana na [[Musa]] kadiri ya [[Biblia]].
 
==Maisha==
Ramses II alikuwa mfalme wa pili wa Nasaba ya 19 ya familia ya kifalme na alikuja kuwa miongoni mwa Mafarao wenye nguvu kuwahi kuwepo Misri.
 
Ramses II alipewa kiti cha Ufalme mapema kwenye umri wa miaka 20 akaongoza kati ya mwaka 1279 KK hadi alipofariki miaka 67 baadae (1213 KK) kwa maradhi ya mishipa, na ini. Hivyo aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya mafarao.
 
Mbali na Vita Ramses II anakumbukwa mno katika juhudi za utunzaji wa Historia ya Misri katika mahekalu ya Ramesseum pamoja na [[Abu Simbel]]. Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo katika mahekalu haya kwa sanamu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Ramses kuwa mmoja wa mafarao muhimu wa Misri ya kale.
 
Jeshi la Ramses lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Mediterania na Libya pia kutoka Wahiti na Wanubia.
 
Pia alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusaini mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga.
 
Katika historia Ramses alishindwa vita mara moja tu! vita inayokumbukwa sana ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria ya leo) mwaka 1274 KK dhidi ya Wahiti. Vilikuwa vita vikubwa vilivyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita vya kale. Ramses alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake, kitu kilichofanya kimojawapo kufyekwa chote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Ramses ikampasa arudi nyuma sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.
 
Vitabu kadhaa vya dini vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza, vikidai kuwa Ramses alifia kwenye maji wakati akiwafukuza Waisraeli. Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi ya kibinadamu. Moja ya ushahidi ni wa Mwili/[[Mumia]] wa Sese ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa!
 
Wengine wanaenda mbali zaidi kuwa Ramses mwili wake huwa hautaki kuzikwa! Kumbe huyo mwanzo alizikwa kwenye kaburi KV7 katika Bonde la Wafalme, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la malkia Inhapy.
 
Miaka mingi baadaye waliuhamishia tena mwili kwenye kaburi la kuhani mkuu Pinudjem II. Yote hii ni sababu ya kumbukumbu katika [[hiroglifi]].
 
Kutokana na matetemeko yaliyoikumba [[Giza (Misri)|Giza]] miaka kati ya miaka [[1000]] hadi [[1500]] [[BK]] vitu vingi vilipotea huku baadhi ya sanamu zikiharibiwa vibaya na matetemeko hayo, na baadhi ya makaburi, majumba, na makumbusho mengine kupotea kabisa! Mwili wa Ramses II nao ukipotea katika matetemeko hayo.
 
Mwanzoni mwa [[miaka ya 1800]], mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Bahari ya Shamu.
 
Ramses II, hakufa kwenye Gharika ya Musa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa [[mzee]], zaidi ya miaka 80 kwa [[maradhi]] ya kawaida.
 
Pia si mwili wa Ramses II tu uliopo kwenye makumbusho ya Misri, ni miili mingi ya Mafarao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Misri ya kale.
 
==Tanbihi==