Hali za mata : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:53, 15 Septemba 2019

Katika fizikia, hali ya maada ni moja kati ya miundo tofauti ambayo maada hupatikana.Hali nne za maada ambazo huoneakana katika maisha yetu ya kila siku ni mango,kiowevu,plasma na gesi. Kihistoria, utofauti huu wa hali za maada unatokana na tofauti za sifa katika tabia za kila hali. Maada katika hali ya mango huchukua ujazo na umbo lisilobadilika, pamoja na chembe zake ambazo ni atomu,molekuli na ioni zikiwa zimeshikamana kwa pamoja katika eneo moja. Maada katika hali ya kiowevu huwa na ujazo usiobadilika, lakini huwa na umbo linalobadilikabadilika kutokana na chombo ilichowekwa.Chembe zake ziko karibukaribu lakini ziko huru. Maada katika hali ya gesi ina ujazo pamoja na umbo mabalo hubadilikabadilika, vyote vikijibadilisha ili kujaza chombo ilichowekwa.Chembe zake haziko karibukaribu wala kukaa mahali pamoja bali huwa huru zikizungukazunguka katika sehemu zilipowekwa.Maada katika hali ya plasma huwa na umbo na ujazo unaobadilika na pia huwa na atomu zisizo na chaji pamoja na idadi kadha ya ioni na elektroni, zote zikiwa na uwezo wa kusogea kwa uhuru.

Hali nne za maada.Kuanzia juu kulia, nazo ni mango, kiowevu,plasma na gesi, zikiwa zimewakilishwa na sananmu ya barafu, tone la maji, mzingo umeme na hewa iliyozunguka mawingu.
Mango fuwele: kielelezo cha kiatomu cha Strontium titanate. Zilizo angavu ni atomu za strontium na nyeusi ni za titanium.