Kipindi cha Pasaka : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 8 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q867783 (translate me)
Holder (majadiliano | michango)
d corr using AWB
Mstari 9:
Katika [[maisha]] ya kawaida watu wanafanya [[sherehe]] mbalimbali, si za [[dini]] tu. [[Sikukuu]] yoyote inatokeza [[furaha]] ya kuishi: usipokuwa na mtazamo wa kuridhika na maisha, kumwaga [[pesa]] katika [[anasa]] hakuondoi [[huzuni]] ya kukata tamaa. Sikukuu yoyote ni [[adhimisho]] la pamoja: inatokana na watu kukubaliana katika kujali mambo fulanifulani au walau kuheshimiana; pia inajenga [[jamii]] kwa kurudisha furaha ya kuwa pamoja.
 
Kwa Wakristo sherehe kuu kuliko zote ni Pasaka: ndiyo sikukuu yenyewe ambayo inadumu siku hamsini mfululizo hadi [[Pentekoste]] na inaitwa Dominika kubwa. Kwa kweli Pasaka si sherehe mojawapo tu wala kipindi kimojawapo tu katika [[mwaka wa liturujia]], bali ndiyo kiini chake, kama vile Dominika (Pasaka ndogo ya kila wiki) ilivyo kiini cha [[juma]] zima. Ni adhimisho la [[uzima mpya]] na wa [[milele ]] aliotushirikisha Kristo mfufuka kwa njia ya [[sakramenti]]: [[ubatizo]] na [[kipaimara]] kwa Wakristo wachanga, [[kitubio]] kwa waliobatizwa zamani, hasa [[ekaristi]] kwa wote; humo hatumkumbuki tu Yesu, bali tunakutana naye, hai tena mtukufu. Adhimisho hilo ni la pamoja kwa sababu tumekuwa [[moyo]] mmoja na [[roho]] moja katika Kristo kwa kumiminiwa Roho Mtakatifu. Kwa [[kumega mkate]] mmoja tunaimarisha [[ushirika]] wetu na kuwajibika kumtambua Yesu katika wale wote tunaokutana nao, hasa [[maskini]].
 
[[Mang’amuzi]] hayo ya imani yanatuchochea kuimba mfululizo, [[Aleluya]]! Bila ya [[shaka]] tunaimba tukiwa njiani kuelekea kwetu: hatujafikia pale tutakapoimba katika [[heri]] ya starehe ya milele. Tunaimba tusije tukalemewa na mzigo wetu wa maisha. [[Augustino wa Hippo]] anatuonya: “Imba anavyofanya [[msafiri]]. Imba lakini tembea, usahau [[uchovu]] wako kwa kuimba, lakini jihadhari na [[uvivu]]. Imba na tembea”. Aleluya inatokeza vizuri furaha na [[tumaini]] letu: ndiyo sababu tunaikariri sana. Pamoja na hayo, uhuru wetu unatudai tuushuhudie kwa matendo na hasa kwa kuwakomboa [[ndugu ]] zetu wanaodhulumiwa.
 
Kristo amefufuka kweli na atatufufua sisi pia: tutaishi naye kwa Baba katika [[umoja]] wa Roho Mtakatifu. Hata sasa yu pamoja nasi (ndiyo maana ya [[mshumaa wa Pasaka]]). Tukiwa naye maisha yanatunogea, kwa kuwa yote yameinuliwa tena na kufanywa mapya. Tumekombolewa kutoka utumwa wa [[dhambi]] na [[mauti]], tumekuwa [[wana wa Mungu]] na kuishi kwa uhuru wa [[upendo]] tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Kristo amekuwa [[Bwana]] na anaendelea kueneza ufalme wake. Hatuwezi kuogopa chochote tena kwa kuwa [[historia]] ni yake yeye aliye [[Alfa na Omega]].