Martin Luther : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 44:
 
===Baada ya kutengwa===
Hivyo Luther alitengwa na Kanisa, lakini wengi walimfuata. Mwaka huohuo Luther aliitwa mbele ya [[Bunge la Ujerumani Germany crused]] ili ajitetee. Ni kwamba sheria za [[Dola Takatifu la Roma]] la Kijerumani zilidai mzushi akamatwe au hata auawe. Alipodaiwa na [[Bunge]] la [[Worms]] akane baadhi ya mafundisho yake, Luther akasimama mbele ya [[Mfalme mkuu]] na wakubwa wote akasema: "Nisipoonyeshwa kwa shuhuda za Biblia, na kwa hoja zinazoeleweka ya kwamba nimekosea, sitakana". Upande wake [[Kaisari]] [[Karolo V]] alitoa [[hotuba]] muhimu akijitambulisha kama mzao wa vizazi vingi vya [[watawala]] walioona daima ni [[wajibu]] wao kutetea imani katoliki «ili kuokoa watu» akasema naye ana wajibu huohuo. Alisisitiza kwamba mtawa mmoja anakosea anapodai kupinga Ukristo wa miaka [[elfu]].
 
Hivyo Bunge hilo ulimhukumu Luther na kuagiza watawala wa maeneo wakomeshe kwa kila namna [[uzushi]] aliouanzisha. Hata hivyo, kwa kuwa hoja za Luther zilikubaliwa na wengi nchini, [[agizo]] hilo halikutekelezwa. Alitangazwa kuwa [[adui]] wa Kanisa na wa [[serikali]] lakini aliruhusiwa kurudi [[Nyumba|nyumbani]]. Maisha yake yalikuwa hatarini lakini mtawala wa eneo lake alimlinda.