Vampiri : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'alt=Vampiri|thumb|Vampiri '''Vampiri''' ni madubwana katika hadithi na hekaya. Hadithi za kwanza za vampiri ziliha...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:49, 17 Novemba 2019

Vampiri ni madubwana katika hadithi na hekaya. Hadithi za kwanza za vampiri zilihadithiwa huko Ulaya Mashariki, lakini watu wengi wanadhani vampiri waliundwa na Bram Stoker katika riwaya maarufu, Dracula. Watu wachache wanaamini kuwa vampiri wanaishi, lakini bado ni maarufu sana katika sinema, televisheni, na vitabu.

Vampiri
Vampiri

Vampiri hapo zamani walikuwa watu lakini wana laana ya kiuchawi. Vampiri lazima wanywe damu ili kuishi. Wao hufanya hivyo kwa kuuma watu au wanyama kwenye shingo na meno yao mawili marefu. Watu ambao wanauliwa na vampiri kwa kunyonywa damu wanaweza pia kuwa vampiri kama wao baada ya kufa. Katika hadithi nyingi, vampiri wanaweza kubadilika kuwa wanyama wengine, kwa kawaida popo, ingawa pia mbwa mwitu, paka au panya.