Ufunuo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 2001:4C4E:1549:B00:D1FA:B06:8135:49FD (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni
Tag: Rollback
Mstari 11:
 
== Namna za kutolewa ==
Namna za ufunuo kufanyika zinawzinaweza kuwa mbalimbali, kama vile:
* Mtu kuinuliwa [[mbinguni]] au kwenda [[kuzimu]];
* Mtu kupata ujumbe kwa njia ya [[ndoto]] [[usingizi|usingizini]] au [[njozi]] wakati wowote;
* Mtu [[kutoka nje ya nafsi]].
 
Kutokana na [[asili]] yake isiyo ya [[Maumbile|kimaumbile]], ufunuo hauwezi kuchunguzwa na mbinu za [[sayansi]]. Hata hivyo ni muhimu kupambanua ufunuo wa kweli na ule bandia ambao mtu anaweza kudanganyika au kudanganya.
 
== Mada ==
Ufunuo unaweza kuhusu:
* matukio yajayo (k.mf. mwisho wa [[dunia]]);
* mambo ya mbinguni kuhusu Mungu, [[malaika]] n.k.;
* ufafanuzi wa matukio ya wakati uleule.
 
== Uyahudi ==
Kadiri ya dini ya Kiyahudi, Mungu alijifunua mara nyingi katika [[historia]] ya [[taifa]] lao kama [[Historia ya Wokovu]], kuanzia [[Babu|mababu]] wao, lakini hasa kumpitia [[Musa]], asili ya [[Torati]] (vitabu vitano vya kwanza vya [[Biblia ya Kiebrania]]).
 
Baada yake walitokea [[manabii]] wengi waliokubalika kuwa wa kweli na ambao vitabu vyao vilipokewa na wengi kama vitakatifu.
 
[[Tanakh]] ilikamilika kwa vitabu vingine vilivyoongezwa kabla ya [[Yesu Kristo]].
 
Wayahudi wanaendelea kumsubiri [[Masiya]] atakayekamilisha ufunuo wao.
 
== Ukristo ==
Wakristo wanapokea ufunuo wa Mungu kwa taifa la [[Israeli]], wakiona ujio wa [[Yesu]] kuwa ndio [[kilele]] chake, ambapo Mungu alijifunua si kwa njia ya manabii, bali kwa njia ya [[Mwana]] wake, aliye [[Neno wa milele]]. Katika yeye ufunuo umekamilika usiweze kuboreshwa tena. Ufunuo huo unajitokeza hasa katika [[Agano Jipya]].
 
Kwa [[imani]] hiyo, Mungu aliwahi kujifunua kwa [[wazazi]] wetu wa kwanza, [[Adamu]] na [[Eva]], akaendelea hasa kwa [[taifa]] la [[Israeli]], hadi alipomtuma [[Mungu Mwana|Mwanae]] ajifanye mtu wa taifa hilo teule. “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana” ([[Eb]] 1:1-2).
 
Baada ya hapo, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani [[Neno la Mungu|Neno]] wake wa [[milele]]. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” ([[Yoh]] 1:17-18). Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” ([[Math]] 24:35). “Ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!” ([[Gal]] 1:8-9).
 
===Msimamo wa Kanisa Katoliki===
Ufunuo huo wa Mungu unatufikia kupitia [[Kanisa]] lake, lililokabidhiwa [[Mapokeo ya Mitume]] na linaloongozwa na [[Roho Mtakatifu]] hadi [[ukweli]] wote. Yesu aliahidi kwamba, “Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yoh 16:13). “Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” ([[1Kor]] 2:10).