Saudia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 151.233.179.208 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na CommonsDelinker
Tag: Rollback
Mstari 59:
 
==Historia==
Jina la nchi limetoka kwa [[familia]] ya watawala, yaani [[familia]] ya aliyeianzisha, [[Chifu]] [[Ibn Saud]] wa [[Riyad]]. Yeye, baada ya kuondoka kwa [[jeshi]] la [[Waturuki]] [[Waosmani]] waliotawala Arabia kwa karne kadha, alishinda [[vita]] baina ya [[Kabila|makabila]] ya Uarabuni ya kati akaweza kuvamia na kutawala maeneo ya [[Najd]] na [[Hejaz]] na mwaka [[1932]] alitangaza [[Ufalme wa Uarabuni wa Saudia]].
 
Kwa maelezo zaidi, Najd ilikuwa ndiyo chanzo cha harakati ya [[Wahabiya]] tangu [[karne ya 18]] walioshikamana na [[nasaba]] ya Saud<ref>[https://www.britannica.com/topic/history-of-Arabia History of Arabia], tovuti ya Encyclopedia Britannica</ref>.
 
[[Mwaka]] [[1744]] [[kiongozi]] wa kikabila [[Muhammad bin Saud]] aliungana na kiongozi wa kidini [[Muhammad ibn Abd al-Wahhab]] na umoja huo wa [[familia]] ya Saud na [[kundi]] la kidini la [[Wahabiya]] uliunda [[utawala]] wa kwanza wa Wasaudi juu ya Riad na sehemu za Najd.
 
Tangu [[1818]] Wasaudi walishindwa katika Najd na [[jeshi]] la [[Waturuki]] [[Waosmani]]; mwaka [[1891]] walipaswa kuondoka Najd na kukimbilia [[Kuwait]].
 
Lakini mwaka [[1902]] [[Abdul Aziz Ibn Saud]] alifaulu kuvamia tena Riad na kuimarisha utawala wake huko. Wakati wa [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia|Vita Kuu ya kwanza]] hakushiriki katika [[vita]] ya [[Waarabu]] dhidi ya Waosmani, badala yake alishindana na [[makabila]] ya Najd ambayo hawakumtambua kama mkuu.
 
Mwaka [[1921]] aliweza kujitangaza kama [[Emir]] wa Najd. Hapo alivamia [[ufalme]] wa [[Hijaz]] akaushinda na mwaka [[1926]] Ibn Saud alijitangaza kuwa mfalme wa Hijaz. Mwaka uliofuata alianza kutumia [[cheo]] cha mfalme pia kwa Najd. Baada ya kutawala sehemu hizo mbili kwa namna ya pekee alitangaza maungano ya falme zote mbili kwenye mwaka [[1932]] akaanzisha Ufalme wa Uarabuni wa Saudia<ref>[http://countrystudies.us/saudi-arabia/7.htm The Saud Family and Wahhabi Islam], Helen Chapin Metz, ed. Saudi Arabia: A Country Study. Washington: GPO for the Library of Congress, 1992</ref>.
 
==Watu==