Tofauti kati ya marekesbisho "Kisukuku"

8 bytes added ,  miezi 8 iliyopita
Tags: Mobile edit Mobile web edit Advanced mobile edit
 
== Visukuku vya kijiwe ==
Mara nyingi [[Mwili|miili]] ya wanyama na mimea imehifadhiwa kwa umbo la jiwe. Ni kama picha au hata [[sanamu]] ya kiumbe kile. Mifano bora imepatikana pale ambapo mmea au mwili wa mnyama ulianguka katika [[matope]] laini na kuzama chini haraka. Ndani ya matope laini mwili haukuoza shauri la uhaba wa [[oksijeni]] na uhaba wa [[bakteria]]. Polepole [[maji]] ya matope yaliingia ndani ya mwili na kujaza nafasi zilizojazwa awali na [[kiowevu]] cha [[seli]] wakati kiumbe kilipokuwa hai. Maji ya matope yalipeleka pia [[minerali]] mbalimbali ndani ya mwili. Jinsi mwendo huu ulivyoweza kuendelea bila kuzuiwa, polepole hata [[seli]] ziliweza kujazwa kwa vipande vidogo vya matope na [[minerali]] nyingine. Kama baada ya miaka mingi matope yalikauka, hata matope ndani ya seli za mwili ulikauka lakini kwa kutunza umbo la seli hizi. Kama [[ganda]] la matope liliendelea kufunikwa na tabaka za [[udongo]] wa juu, [[shindikizo]] la juu lilianza kubadilisha ule udongo kuwa [[jiwe]] na [[mwamba mashapo]] kabisa.
 
Kama mwili wenyewe umeshaoza hadi [[kiunzi]] cha [[mifupa]] kilifunikwa kuna pia visukuku vya mifupa tu. Viumbe kama [[konokono]] mara nyingi viliacha visukuku vya umbo la nje pekee, kwa sababu miili yao ni laini sana, hivyo ilipotea haraka, na ganda lao halikubali maji yenye minerali kuingia ndani yake.