Tofauti kati ya marekesbisho "Mtihani"

1 byte added ,  mwaka 1 uliopita
no edit summary
Mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani.Kama tujuavyo, lengo la mtihani kwa mwanafunzi ni kumpima kile alichojifunza kutoka chanzo cha mafunzo yake, baada ya kipimo hicho ndipo mwanafunzi anaweza kufanyiwa tathmini ya kumjua kama anafaa kwa lipi na hafai kwa lipi. Kitaaluma, hasa katika masuala ya shule, mwanafunzi anaweza kupimwa katika vipindi vikuu vitatu:
 
- '''Kabla ya kujiunga na shule au taasisi:''' Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia alama za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mitihani ya namna hii wengi huiita usaili.
- '''Katikati ya masomo au mafunzo:''' Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hii huweza kutolewa kwa ratiba za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hii ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake.