Mtihani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6:
 
- '''Kabla ya kujiunga na shule au taasisi:''' Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia alama za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mitihani ya namna hii wengi huiita usaili.
 
- '''Katikati ya masomo au mafunzo:''' Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hii huweza kutolewa kwa ratiba za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hii ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake.
 
- '''Mwisho wa masomo/mafunzo:''' Mara baada ya kumaliza masomo au mafunzo mwanafunzi hupewa mtihani ili kumpima juu ya yale yote aliyojifunza. Kwa baadhi ya nchi au nchi nyingi duniani hutumia mitihani ya mwisho kama ni upimaji utakaomwezesha mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu mafunzo yake. Maranyingi, kushindwa kwa mtihaani wa mwisho ni kushindwa kwa masomo yake. Mitihani ya namna hii hutolewa na taasisi maalumu kama vile Baraza la mitihani la Taifa kwa nchi ya Tanzania na taasisi nyingine zenye dhamana ya kufanya hivyo.