Mtihani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 5:
Hivyo mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani. Kama tujuavyo, lengo la mtihani kwa mwanafunzi ni kumpima kile alichojifunza kutoka chanzo cha mafunzo yake, baada ya kipimo hicho ndipo mwanafunzi anaweza kufanyiwa tathmini ya kumjua kama anafaa kwa lipi na hafai kwa lipi.
 
==Aina za mitihani shuleni==
Kitaaluma, hasa katika masuala ya shule, mwanafunzi anaweza kupimwa katika vipindi vikuu vitatu:
 
# Kabla ya kujiunga na shule au taasisi: Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au [[taasisi]] hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia [[alama]] za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga nayo. Mitihani ya namna hiyo wengi huiita [[usaili]].
 
# Katikati ya masomo au mafunzo: Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hiyo huweza kutolewa kwa [[ratiba]] za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hiyo ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake. Katika mitihani [[asilimia]] kubwa ya wanafunzi huwa na [[woga]], ndiyo maana hupewa mitihani shuleni ili waizoee. Katika shule huwa na mashindano ya wanafunzi ili waweze kumpata wa kwanza kati yao. Mitihani hutungwa na walimu wenyewe. Huwa na mtihani wa [[wiki]], [[mwezi]], [[robo]] [[mhula]], [[nusu]] mhula na mtihani wa mwisho.
 
# Mwisho wa masomo/mafunzo: Mara baada ya kumaliza masomo au mafunzo mwanafunzi hupewa mtihani ili kumpima juu ya yale yote aliyojifunza. Kwa baadhi ya nchi au nchi nyingi [[duniani]] hutumia mitihani ya mwisho kama ni upimaji utakaomwezesha mwanafunzi kupata [[cheti]] cha kuhitimu mafunzo yake. Mara nyingi, kushindwa kwa mtihani wa mwisho ni kushindwa kwa masomo yake. Mitihani ya namna hiyo hutolewa na taasisi maalumu kama vile Baraza la Mitihani la Taifa kwa nchi ya [[Tanzania]] na taasisi nyingine zenye dhamana ya kufanya hivyo. Nchini [[Tanzania]] kuna [[mtihani wa taifa]]: mtihani huo humvusha mwanafunzi katika [[daraja]] alilopo na kwenda katika hatua nyingine (kutoka [[shule ya msingi]] kwenda [[sekondari]], kutoka sekondari kwenda [[chuo kikuu]] na hatimaye kufaulu na kutimiza malengo yake).