Wawanji : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 19:
==Dini na ushirikina==
[[Idadi]] kubwa ya Wawanji ni [[Wakristo]], wanamwamini [[Yesu Kristo]]. Pia [[Waislamu]] wapo, lakini si kwa idadi kubwa: kila watu 10 Mwislamu ni mmoja au hakuna kabisa. Hii inajidhihirisha wazi kutokana na kuwepo kwa [[Kanisa|makanisa]] mengi kuliko [[misikiti]], mfano [[mji]] wa [[Matamba]] una msikiti mmoja ambao unafanana na [[nyumba]] ya mtu ya kuishi eneo la Mahanji, lakini makanisa ni mengi mno, yapo kila [[kitongoji]].
 
Pia Wawanji wanasadikika kuwa [[Ushirikina|washirikina]] toka enzi; ushirikina wao ni wa pekee, unatofautiana na makabila yote Tanzania, na unajulikana kama Wanyambuda. Ushirikina huo umesambaa na unakua na kuenea kwa kasi zaidi [[miaka ya 2010]]. Zamani walikuwa ni [[wazee]] lakini miaka hii mpaka [[vijana]] wanaomaliza [[elimu]] za [[sekondari]] wanapewa aina hii ya ushirikina. [[Kazi]] yao kubwa ni kula watu, yaani wanaamini kuwa wanaweza wakakuua [[Uchawi|kiuchawi]] na ukaendelea kuishi hata zaidi ya [[wiki]], huku wakiwa tayari wameshakula vitu vya ndani kama [[ulimi]], [[utumbo]] na [[ini]]. Hivyo [[mgonjwa]] anaweza akalazwa [[hospitali]], kumbe ameshaliwa [[kiungo|viungo]] vyake vya ndani.
 
Wana [[sayansi]] ya ajabu ambayo huwezi kuona hata walipotolea hiyo [[nyama]] ila kuna wazee [[wataalamu]] ndio hutambua hilo mapema na wanawajua mpaka waliohusika. Uchawi huo huenezwa kutoka [[familia]] moja kwenda nyingine kwa njia ya [[pombe]] kwenye [[Kilabu|vilabu]] vya kienyeji. Hata kama ulikuwa mtu mwema, kama ni mnywaji wa pombe za kienyeji unakuwa kwenye hatari ya kupata huo uchawi.
 
Lakini hawa Wanyambuda hawawezi kumuua mgeni au mtu wasiyemjua, ila wanachokifanya ni kila mshirika ambaye yupo kwenye hicho kikundi cha Unyambuda anatoa [[sadaka]] ya mtu ampendaye kutoka katika familia yake: anaweza kumtoa [[mtoto]] wake mpendwa, au [[mama]] yake, au [[mke]] wake, au hata [[mjomba]] na [[shangazi]] ili mradi ana [[undugu]] naye. Kikundi kinapendekeza mtu ambaye ni mpendwa kwako, ikitokea unashindwa kutoa sadaka, basi kikundi kinapendekeza kukuua mwenyewe, na lazima uawe tu.
 
Hii hali imepelekea kuhama kwa vijana pindi tu wanapomaliza elimu zao za sekondari, kwani kijana aliYesoma na anaYeonekana ni msaada mkubwa kwa familia yake, huyo ndiye kipaumbele kikubwa kutolewa sadaka na [[wazazi]] wake au [[ndugu]] zake. Hii imepelekea vijana wengi kuhamia mjini na waliofanikiwa kimaisha wanashindwa kutoa msaada nyumbani kwao au hata kuwajengea wazazi wao nyumba nzuri, wakihofiwa kuuawa na mzazi au mtoto mwenyewe.
Kwa jina lingine wanaitwa [[Freemasons]] wa Uwanji.
 
==Tanbihi==