Wawanji : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
No edit summary
Mstari 1:
'''Wawanji''' ni [[kabila]] kutoka [[wilaya]] ya [[Makete]], katika [[milima ya Kipengere]] ya [[Mkoa wa Njombe]], sehemu ya [[kusini]] ya nchi [[Tanzania]].
 
[[Mwaka]] [[2003]] [[idadi]] ya Wawanji ilikadiriwa kuwa 28,000<ref>[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=wbi Vwanji. A language of Tanzania.]</ref>. [[Lugha]] yao ni [[Kiwanji]].
 
Wawanji ni majirani kabisa wa kabila la [[Wakinga]]. Wawanji na Wakinga wamepakanishwa na [[hifadhi ya Kitulo]]. [[Asilimia]] kubwa ya Wawanji wapo sehemu za [[Ikuwo]] na [[Matamba]], maarufu kama [[bonde]] la Uwanji.
Mstari 8:
Inasemekana Wawanji walitokea [[Dodoma]] katika kabila la [[Wagogo]]; [[uthibitisho]] wa hilo ni kwamba ma[[jina]] mengi ya koo za Kigogo na Kiwanji zinafanana. Tofauti ipo katika matamshi ambayo yaliathiriwa na [[lafudhi]] ya mahali walipofika wazee wa zamani walipotoka [[Ugogo]] kwenda [[kusini]]. Kwa mfano, Wagogo wana Msemwa ila Wawanji wana Nsemwa, Wagogo wana Mgogo ila Wawanji wana Ngogo, Wagogo wana Mkinda ila Wawanji wana Nkinda. Hii inaonyesha jinsi gani asili ya watu hao ilivyo moja, ila imebadilika kutokana na [[uhamaji]] ambao ni moja ya [[tabia]] ya [[viumbe hai]]. Kwa maana hiyo, ukitaka kuita majina ya koo za Kiwanji mengi yanaanza na N'.
 
Baadhi ya koo za wawanji ni hizi;: Mbwanji, Nguvila, Ngogo, Nkinda, Malila, Mbena, Mbala, Sanga, Chaula, Chawe, Mbena, Mboka, Mahali, Konga, Ngao, Mboka, Nyambo, Mbwilo, Malila nkn.k.
 
==Mahusiano ya Wawanji na makabila mengine==
Mstari 20:
 
==Dini na ushirikina==
[[Idadi]] kubwa ya Wawanji ni [[Wakristo]], wanamwamini [[Yesu Kristo]]. Pia [[Waislamu]] wapo, lakini si kwa idadi kubwa: kila watu 10 Mwislamu ni mmoja au hakuna kabisa. Hii inajidhihirisha wazi kutokana na kuwepo kwa [[Kanisa|makanisa]] mengi kuliko [[misikiti]], mfano [[mji]] wa [[Matamba]] una msikiti mmoja ambao unafanana na [[nyumba]] ya mtu ya kuishi eneo la Mahanji, lakini makanisa ni mengi mno, yapo kila [[kitongoji]].
 
Pamoja na hayo, [[ushirikina]] unajitokeza sana.
 
==Tanbihi==
<references/>
 
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{Makabila ya Tanzania}}
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{DEFAULTSORT:Wanji}}
 
[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Wilaya ya Makete]]