Tofauti kati ya marekesbisho "Uhindi"

2,043 bytes added ,  miezi 4 iliyopita
no edit summary
 
 
== Historia ==
===Historia ya awali===
[[Binadamu]] walifika India kutoka [[Afrika]] kabla ya miaka 55,000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama [[wawindaji-wakusanyaji]] waliozagaa [[Bara|barani]], umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa [[DNA|urithi wa kibiolojia]], ambayo inapitwa na Waafrika tu.
 
Makazi ya kudumu yalianza [[magharibi]], katika [[beseni]] la [[mto Indus]], miaka 9,000 iliyopita, hata kuzaa [[ustaarabu]] maalumu (Indus Valley Civilisation) katika [[milenia ya 3 KK]].
 
===Kabla ya ukoloni===
Kufikia [[mwaka]] [[1200 KK]], [[Kisanskrit cha Kale]], mojawapo kati ya [[lugha za Kihindi-Kiulaya]], kilikuwa kimeenea India kutoka [[Kaskazini]]-Magharibi, kikawa [[lugha]] ya [[Rigveda]], mwanzoni mwa [[dini]] ya [[Uhindu]]. Hivyo [[lugha za Kidravidi]] zikakoma kaskazini.
 
Kufikia mwaka [[400 KK]], [[tabaka|matabaka]] ya kudumu katika [[jamii]] yalikuwa yamejitokeza katika Uhindu. Hapo dini za [[Ubuddha]] na [[Ujaini]] zilitokea, zikipinga taratibu hizo za kibaguzi. Katika [[bonde]] la [[mto]] [[Gange]] yalianza [[madola]] ya [[dola la Maurya|Maurya]] na [[Dola la Gupta|Gupta]]. Ndani yake hadhi ya [[wanawake]] ilirudi nyuma, na mtazamo wa kwamba baadhi ya watu hawatakiwi hata kuguswa ukaimarika. Huko India [[Kusini]], Falme za Kati zilieneza [[maandishi]] na [[tamaduni]] vya lugha za Kidravidi kwa [[Ufalme|falme]] za Asia Kusini [[Mashariki]].
 
Kati [[karne]] za kwanza baada ya [[Kristo]], dini za [[Ukristo]], [[Uislamu]], [[Uyahudi]] na [[Uzoroastro]] pia zilitia mizizi katika [[pwani]] za Kusini.
 
[[Majeshi]] kutoka [[Asia ya Kati]] yalivamia kwa [[kwikwi]] mabonde ya India, hata kuunda [[usultani]] wa [[Delhi]] na kuingiza India Kaskazini katika [[umma]] wa Kiislamu.
 
Katika [[karne ya 15]] [[BK]], [[Dola la Vijayanagara]] liliunda utamaduni wa kudumu wa Kihindu kusini mwa India. Katika [[Punjab]], [[Usikh]] ulianzishwa, ukipinga [[dini rasmi]].
 
[[Dola la Mughal]], mwaka [[1526]], liliwezesha karne mbili za [[amani]] na kuacha [[urithi]] wa [[usanifu majengo]] bora.
 
===Wakati wa ukoloni===
{{main|Uhindi wa Kiingereza}}