Mauti : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
kinyume na uumbaji
Tags: Replaced blanking Mobile edit Mobile web edit
Mstari 1:
kifo ni kinyume uumbaji kwa mujibu dini ya kikristo. maana kanuni ya uumbaji inasema mavumbi-pumzi ya uhai=kifo
[[File:Skullclose.jpg|thumb|upright=1.3|[[Fuvu la kichwa]], [[ishara]] maarufu ya kifo.]]
[[File:Kuoleman Puutarha by Hugo Simberg.jpg|alt=|thumb|Mauti ikishughulikia maua yake, katika Kuoleman puutarha, kazi ya Hugo Simberg (1906).]]
[[File:All causes world map-Deaths per million persons-WHO2012.svg|thumb|upright=1.4|[[Idadi]] ya vifo kati ya watu [[milioni]] moja mwaka [[2012]]{{refbegin|3}}{{legend|#ffff20|1054-4,598}}{{legend|#ffe820|4,599-5,516}}{{legend|#ffd820|5,517-6,289}}{{legend|#ffc020|6,290-6,835}}{{legend|#ffa020|6,836-7,916}}{{legend|#ff9a20|7,917-8,728}}{{legend|#f08015|8,729-9,404}}{{legend|#e06815|9,405-10,433}}{{legend|#d85010|10,434-12,233}}{{legend|#d02010|12,234-17,141}}{{refend}}
]]
'''Mauti''' (kutoka [[Kiarabu]] '''موت''', ''maut'') au '''kifo''' (kutoka [[kitenzi]] cha [[Kibantu]] ''kufa'') ni [[mwisho]] wa [[uhai]]; kwa [[lugha]] ya [[biolojia]] mwisho wa michakato yote ndani ya [[kiumbehai]] ambayo ni [[dalili]] za uhai.
 
==Chanzo==
Mauti hutokea kutokana na sababu mbalimbali kama vile
* [[umri]] mkubwa unaosababisha michakato ya kimsingi [[Mwili|mwilini]] kusimama polepole
* [[muda]] mrefu wa maisha unaoruhusu makosa na kasoro kujumuika na kusababisha madhara (mfano: [[kansa]])
* [[magonjwa]] yanayovuruga michakato ya uhai hadi kuisimamisha
* [[ajali]] zinazoharibu [[viungo]] muhimu mwilini
* ukosefu wa [[chakula]], [[maji]], [[hewa]] au kinga dhidi ya [[mazingira]] magumu
* athari haribifu kutoka viumbe wengine (k.m. kushambuliwa) au kutoka mazingira
 
==Hakikisho==
Kwa [[binadamu]] kutokea kwa kifo mara nyingi hakutokei mara moja; katika mazingira ya kawaida kifo kinaonekana kama [[moyo]] hausikiki tena na [[mapafu]] hayakupumua kwa [[dakika]] kadhaa.
 
Hata hivyo kuna uwezekano wa kwamba [[kazi]] ya moyo na mapafu ni hafifu kiasi kwamba haitambuliki. Penye [[hospitali]] nzuri na mitambo ya kiganga mara nyingi mtu anarudi kuishi ingawa mahali pengine ametazamwa ameshaaga [[dunia]]. Kama [[mashine]] zinaendelea kuchukua kazi ya moyo na mapafu si rahisi kujua kifo kinatokea lini.
 
[[Wataalamu]] wengi siku hizi wanapoona michakato ya kawaida ya [[ubongo]] imekwisha kwa muda fulani, wanasema kifo kimetokea. Hata hivyo kuna kesi za watu wanaozinduka baada ya muda huo.
 
== Mauti na utamaduni ==
Katika [[utamaduni]] na [[imani]] za watu mauti ni jambo muhimu. Lugha ina njia nyingi za kuitaja kwa mfano kuaga dunia, kufariki dunia n.k.
 
Katika [[dini]] na [[falsafa]] kuna misimamo mbalimbali kuhusu mauti kama vile
# Mauti ni mwisho wa binadamu kimwili na kiroho; hakuna kinachobaki baada ya kifo
# Mauti ni hatua tu katika [[mzunguko wa maisha]]; [[nafsi]] au [[roho]] inarudi katika [[maumbile]] mengine
# Kifo ni kupita penginepo: [[uzima wa milele]], [[mbinguni]], upeo wa wafu n.k.
 
==Katika Ukristo==
Hasa kadiri ya [[Ukristo]], ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea [[neema]] tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” ([[Eb]] 9:27). “Katika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatima” ([[YbS]] 7:36). “Hamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka” ([[Yak]] 4:14). “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” ([[Math]] 26:41).
 
“Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” ([[Zab]] 116:15). Hasa [[utiifu]] wa [[Yesu]] [[Msalaba|msalabani]] umegeuza [[laana]] ya kifo iwe [[baraka]] kwa waamini wake. “Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” ([[Ufu]] 14:13).
 
Tutakapofariki [[dunia]] [[roho]] yetu isiyokufa, mbali na [[mwili]] unaooza, itapewa [[tuzo]] au [[adhabu]] tuliyostahili kwa [[maisha]] yetu. “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake” ([[Lk]] 16:22-23). “Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” ([[Fil]] 1:21,23). “Nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” ([[2Kor]] 5:8). Kwa kuwa kifo ni “mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” ([[Mhu]] 12:7). [[Kiyama|Siku ya ufufuo]] roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya [[uzima]] au [[moto]] wa [[milele]]. “Pumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno” ([[Ez]] 37:10).
 
{{mbegu}}
 
[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Dini]]
[[Jamii:Uyahudi]]
[[Jamii:Ukristo]]
[[Jamii:Uislamu]]
[[Jamii:Utamaduni]]