Nzige-jangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Uainishaji | rangi = pink | jina = Nzige-jangwa | picha = Copulating desert locust pair.jpg | upana_wa_picha = 250px | maelezo_ya_picha = Jike na dume ya nzig...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:05, 5 Februari 2020

Nzige-jangwa
Jike na dume ya nzige-jangwa (Schistocerca gregaria) wakipandana
Jike na dume ya nzige-jangwa (Schistocerca gregaria) wakipandana
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Caelifera (Wadudu kama panzi)
Familia: Acrididae (Panzi)
Jenasi: Schistocerca
Stål, 1873
Spishi: S. gregaria
(Forskål, 1775)

Nzige-jangwa ni wadudu wa kundi la panzi katika familia Acrididae wa oda Orthoptera ambao wanaishi katika jangwa kwa kawaida. Lakini wakiwa wengi sana hujikusanya katika makundi makubwa na kusafiri mbali ndefu hata nje ya jangwa. Tauni za nzige-jangwa wametishia uzalishaji wa kilimo katika Afrika, Mashariki ya Kati, na Asia kwa karne nyingi. Riziki za angalau moja ya kumi ya idadi ya watu duniani yanaweza kuathiriwa na wadudu hao walafi.

Mzunguko wa maisha

Mzunguko wa maisha wa nzige-jangwa una hatua saba: yai, hatua 5 za tunutu, wanaojulikana kama warukaji, na mpevu mwenye mabawa. Kupandana hufanyika wakati dume aliyekomaa anaporuka juu ya mgongo wa jike aliyekomaa na kumbokora mwili wake kwa miguu. Manii huhama kutoka ncha ya fumbatio ya dume kwenda ncha ya ile ya jike, ambapo huhifadhiwa. Mchakato huo unachukua masaa kadhaa na uingizwaji mmoja wa manii unatosha kwa idadi ya vibumba vya mayai.

Kisha jike hutafuta udongo laini unaofaa kwa kutaga mayai yake. Lazima uwe na joto sahihi na kiwango kizuri cha unyevu na kuwa karibu na majike wengine wanaotaga. Anachunguza mchanga kwa fumbatio yake na kuchimba kishimo ambacho ndani chake anaweka kibumba cha mayai kilicho na mayai hadi mia moja. Kibumba cha mayai kina urefu wa sm 3 hadi 4 (inchi 1.2-1.6) na ncha ya chini ni takriban sm 10 (inchi 4) chini ya uso wa ardhi. Mayai yamezungukwa na povu na hii inakauka mpaka kuwa utando na kuziba kishimo juu ya kibumba cha mayai. Mayai huchukua unyevu kutoka kwa mchanga unaozunguka. Kipindi cha kuatamia kabla ya kujiangua kwa mayai kinaweza kuwa wiki mbili au zaidi sana, kulingana na nyuzijoto.

Baada ya kutoka kwenye yai tunutu mpya huanza kujilisha punde si punde na, ikiwa ana awamu ya kukaa pamoja na wenzake, anavutiwa na tunutu wengine na wanajikusanya. Wakati wa ukuaji anahitaji kuambua ngozi (kuacha kiunzi-nje chake) mara kwa mara. Ganda lake gumu la nje linapasuka na mwili wake unatanuka wakati kiunzi-nje kipya bado ni chororo. Hatua kati ya maambuaji zinaitwa “instars” na tunutu wa nzige-jangwa hupitia maambuaji matano kabla ya kuwa mpevu mwenye mabawa. Tunutu wa awamu ya kukaa pamoja huunda makundi yanayojilisha, kukota jua na kusonga mbele katika vikosi vinavyoshikamana, wakati wale wa awamu ya kutokaa pamoja hawaundi makundi.

Baada ya uambuaji wa tano mdudu anasemekana kuwa mpevu lakini bado hajakomaa kabisa. Kwanza ana rangi ya pinki na hawezi kukuza mayai au kuzalisha manii. Kufikia ukomavu kunaweza kuchukua wiki mbili hadi nne wakati uwepo wa chakula na hali ya hewa zinafaa, lakini kunaweza kuchukua muda mrefu kama miezi sita wakati hali hizo ni duni. Madume hukomaa kwanza na kutoa harufu ambayo huchochea kukomaa kwa majike (feromoni). Wakikomaa wadudu hao wanageuka kuwa njano na fumbatio ya majike huanza kuvimba na mayai yanayokua.

Ekolojia na kuunda makundi

Nzige-jangwa wana awamu mbili: awamu ya "solitaria" na awamu ya "gregaria" (polyphenism). Imeonyeshwa kuwa tunutu na wapevu wa nzige wanaweza kutenda kama gregaria ndani ya masaa machache baada ya kuwekwa katika hali ya msongano, ingawa mabadiliko ya kimofolojia huchukua maambuaji kadhaa ili kuonekana. Nzige wa gregaria wanahitaji kizazi kimoja au zaidi ili kuwa solitaria wakikuzwa katika upweke.

Kuna tofauti katika mofolojia na mwenendo kati ya awamu hizo mbili. Katika awamu ya solitaria tunutu hawaundi makundi lakini huzunguka peke yao. Rangi yao kwanza ni kijani, lakini hatua zinazofuata zinaweza kuwa hudhurungi ikiwa uoto kijani huadimika au kukosekana. Wapevu wa solitaria huruka usiku na kuwa hudhurungi ili kufichika katika mazingira yao na wanaweza kuwa njano isiyoiva wakikomaa.

Katika awamu gregaria tunutu hujikusanya pamoja. Hatua ya kwanza ni nyeusi, zile za pili na tatu ni nyeusi na nyeupe na hatua zinazofuata ni njano kali pamoja na mabaka meusi. Wapevu wasiokomaa ni pinki na waliokomaa ni njano. Wanaruka wakati wa mchana katika makundi mazito.

Badiliko kutoka kwa mdudu wa solitaria asiye msumbufu kwenda kwa mdudu mlafi wa gregaria hufuata kwa kawaida kipindi cha ukame, wakati mvua inanyesha na mimea inaibuka katika maeneo makuu ya uzalishaji wa nzige. Idadi ya wadudu inazidi haraka na mashindano kwa chakula huongezeka. Kadiri tunutu wanaposongamana, changamano ya karibu ya miili yao husababisha miguu yao ya nyuma kugongana. Kichocheo hiki husababisha mfululizo wa mabadiliko ya metaboliki na ya mwenendo ambayo husababisha wadudu kubadilika kutoka kwa awamu ya solitaria kwenda kwa ile ya gregaria.

Wakati tunutu wanapokuwa gregaria, rangi yao hubadilika kutoka kwa kijani hadi njano na nyeusi, na wapevu hubadilika kutoka hudhurungi hadi pinki (wasiokomaa) au njano (waliokomaa). Mwili wao huwa mfupi zaid na wanatoa feromoni inayowafanya wavutiane, ambayo huongeza uundaji wa makundi. Feromoni ya tunutu ni tofauti na ile ya wapevu. Wanapofunuliwa na feromoni ya wapevu, tunutu huchanganyikiwa na kufadhaika, kwa sababu inaonekana kwamba hawawezi "kunusana", ingawa vichocheo vya kuona na kugusa vinabaki. Baada ya siku chache makundi ya tunutu hutengana na wale wanaotoroka umbuai huwa solitaria tena. Inawezekana kwamba athari hii inaweza kusaidia udhibiti wa nzige katika miaka ijayo. CHANGE

Picha