Wahaya : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
No edit summary
Mstari 11:
Wahaya ni maarufu kwa [[uzalishaji]] wa [[ndizi]] na [[kahawa]]. Ni kabila ambalo hupenda sifa, kujisifu na kusifiwa. Pia kabila hilo halitasahaulika kwa jinsi walivyopata shida [[mwaka]] [[1978]] kutokana na [[vita vya Kagera]].
 
Elimu: kuingia kwa [[wamisionari]] katika [[karne ya 19]] ambao walianzisha [[shule]] nyingi za awali na za kati ambapo ilibidi mtu [[Ubatizo|abatizwe]] ili aweze kupata [[elimu]]. [[Wazazi]] wengi walipeleka [[watoto]] wao kubatizwa na hapo kukaanza mvutano, sababu wamisionari walikuwa [[Wakatoliki]] kutoka [[Ufaransa]] na [[Uswisi]] na [[Walutheri]] kutoka [[Ujerumani]] na [[Uholanzi]]. Ndipo kukaanza mashindano ya kuanzisha shule nyingi ili kupata waumini wengi.
 
Wamisionari pia wakawa mstari wa mbele kufungua [[hospitali]] nyingi kila wilaya na [[chuo cha ufundi|vyuo vya ufundi]].
 
Ndiyo maana maeneo hayo ya Kagera elimu ni ya juu kwa wakazi wake na huduma za [[afya]] kuliko mikoa jirani. Na [[kilimo]] cha [[kahawa]] kiliwapa wenyeji fedha za kujenga [[nyumba]] bora na kupeleka watoto wao kwenye elimu ya juu zaidi. Pia kulianzishwa chama cha ushirika cha [[mkoa]] ambacho kilianzisha shule za watoto wa [[wakulima]] kuwasomesha na kutoa mikopo. Eneo hilo lilizidi kurutubishwa kushinda maeneo mengine mengi ya nchi kutoa Uchagga.
 
Pia wamisionari walianzisha [[seminari]] na chuo cha kutoa [[Padri|mapadri]] wao wenyewe.
 
[[Waarabu]] walioleta [[Uislamu]] walikuwa wanakazania sana [[biashara]], si shughuli za [[maendeleo]] ya watu.
{{Makabila ya Tanzania}}
{{mbegu-utamaduni-TZ}}