Nzige-jangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Nyongeza matini
dNo edit summary
Mstari 23:
Mzunguko wa maisha wa nzige-jangwa una hatua saba: [[yai]], hatua 5 za [[tunutu]], wanaojulikana kama warukaji, na mpevu mwenye mabawa. Kupandana hufanyika wakati dume aliyekomaa anaporuka juu ya [[mgongo]] wa jike aliyekomaa na kumbokora [[mwili]] wake kwa [[mguu|miguu]]. [[Manii]] huhama kutoka ncha ya [[fumbatio]] ya dume kwenda ncha ya ile ya jike, ambapo huhifadhiwa. Mchakato huo unachukua masaa kadhaa na uingizwaji mmoja wa manii unatosha kwa vibumba vitatu vya mayai.
 
Kisha jike hutafuta udongo laini unaofaa kwa kutaga mayai yake. Lazima uwe na joto sahihi na kiwango kizuri cha unyevu na kuwa karibu na majike wengine wanaotaga. Anachunguza mchanga kwa fumbatio yake na kuchimba kishimo ambacho ndani chake anaweka kibumba cha mayai kilicho na mayai hadi mia moja. Kibumba cha mayai kina urefu wa sm 3 hadi 4 (inchi 1.2-1.6) na ncha ya chini ni takriban sm 10 (inchi 4) chini ya uso wa ardhi. Mayai yamezungukwa na povu na hii inakauka mpaka kuwa utando na kuziba kishimo juu ya kibumba cha mayai. Mayai huchukua unyevu kutoka kwa mchanga unaozunguka. Kipindi cha kuatamia kabla ya kujiangua kwa mayai kinaweza kuwa wiki mbili au zaidi sana, kulingana na nyuzijoto.
 
[[Picha:S. gregaria dense hopper band.jpg|thumb|left|Kundi zito la tunutu nchini Sudani]]