Nzige-jangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
Nyongeza matini
Mstari 60:
 
Kwa sasa njia kuu ya kudhibiti uvamizi wa nzige-jangwa ni kutumia [[kiuadudu|viuawadudu]], haswa [[fosfati]] ogania kama [[w:fenitrothion|fenitrothion]], [[w:malathion|malathion]] na [[w:chlorpyrifos|chlorpyrifos]]. Hivi vinapulizwa kwa vipimo vidogo vya [[ukolevu]] wa juu kwa [[chombo cha kupulizia|vyombo vya kupulizia]] vilivyopandishwa kwenye [[gari|magari]] au [[ndege (unanahewa)|ndege]] kwa viwango vya matumizi vya [[mjao]] wa chini kabisa ([[w:Ultra-low volume|ultra-low volume]] au ULV). Mdudu hupata kiuawadudu moja kwa moja au kupitia uokotaji wa sekondari (yaani kukanyaga au kula mabaki kwenye mimea). Udhibiti hufanywa na [[shirika|mashirika]] ya [[serikali]] katika nchi zilizoathirika na nzige au na mashirika maalum kama vile Shirika la Udhibiti wa Nzige-Jangwa kwa Afrika ya Mashariki ([[w:Desert Locust Control Organization for East Africa|Desert Locust Control Organization for East Africa]] au DLCO-EA).
 
Nzige-jangwa ana maadui wa asili kama vile [[nyigu]] na [[nzi]] mbuai, nyigu [[kidusia|vidusia]], [[lava]] wa [[mbawakawa]], [[ndege (biolojia)|ndege]] na [[mtambaazi|watambaazi]]. Hao wanaweza kuwa na ufanisi katika kudhibiti idadi ya wadudu wa solitaria lakini wana athari ndogo dhidi ya nzige-jangwa wa gregaria kwa sababu ya idadi kubwa sana ya wadudu katika makundi ya wapevu na ya tunutu.
 
Mara nyingi wakulima hujaribu njia za kimakanika za kuua nzige kama vile kuchimba [[mtaro|mitaro]] na kuzika makundi ya tunutu, lakini hii inahitaji kazi nyuingi na ni ngumu kufanya wakati uvamizi mkubwa umetawanyika kwenye eneo kubwa. Wakulima pia hujaribu kuogofya makundi ya nzige mbali na mashamba yao kwa kufanya kelele, kuchoma tairi au njia nyingine. Hii inaelekea kuhamisha shida kwenye mashamba jirani, na makundi ya nzige yanaweza kurudi tena kwa urahisi kwenye mashamba yaliyotembelewa hapo awali.
 
===Dawa za kibiolojia===
[[Dawa ya kibiolojia|Dawa za kibiolojia]] zinajumuisha [[kuvu]], [[bakteria]], [[uto]] wa [[mbegu]] za [[mwarobaini]] na feromoni. Ufanisi wa dawa nyingi za kibiolojia ni sawa na ule wa dawa za kemikali za kawaida, lakini kuna tofauti. Kwa ujumla dawa za kibiolojia huchukua muda mrefu zaidi kuua wadudu, [[gugu|magugu]] au [[ugonjwa|magonjwa]] ya mimea, kwa kawaida kati ya siku 2 na 10.
 
Kuna aina mbili za dawa za kibiolojia, biokemikali na vijidudu. Dawa za biokemikali ni sawa na kemikali zinazotokea kwa asili lakini zina sumu isiyo kali sana au hazina sumu, kama vile feromoni zinazotumiwa kupata wenzake wa jinsia nyingine. Dawa za kibiolojia zenye vijidudu zina bakteria, kuvu, [[mwani|miani]] au [[virusi]] ambayo inatokea kwa asili au imebadilishwa vinasaba. Kuvu viuawadudu hukandamiza wasumbufu kwa uambukizaji kwa ujumla: kusababisha ugonjwa ambao ni maalum kwa wadudu.
 
==Picha==