Travis Scott : Tofauti kati ya masahihisho

Rapa wa Marekani, mwimbaji, na producer
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Infobox musical artist 2|Jina=Travis Scott|picha=Travis Scott April 2017.jpg}} '''Jacques Berman Webster II''' (kuzaliwa Aprili 30, 1992) anajulikana...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:34, 16 Februari 2020

Jacques Berman Webster II (kuzaliwa Aprili 30, 1992) anajulikana pia kama Travis Scott ambalo ni jina lake la kazi. Huyu ni mwanamuziki wa kimarekani, mwandishi, rapa na mtayarishaji wa muziki. Mnamo mwaka 2012 Travis aliweka mkataba na lebo ya Epic Records. Mnamo mwezi wa Novemba mwaka huo huo alijiunga na lebo ya GOOD Music inayomilikiwa na msanii Kanye West kama sehemu ya utayarishaji wa muziki katika lebo hiyo. Ilipofika mwezi Aprili 2013, alijiunga na kikundi kingine cha Grand Hustle kilichomilikiwa na msanii TI.

Travis Scott
Faili:Travis Scott April 2017.jpg
Taarifa za awali

Travis aliachilia wimbo wake uliojulikana kama mixtape Owl Pharaoh mnamo mwaka 2013, na kufuatiwa na wimbo mwingine uliojulikana kama Days Before Rodeo mwezi Agosti mwaka 2014. Albamu yake ya Rodeo iliweza kutamba kwa wimbo uliojulikana kama "Antidote". Albamu yake ya pili iliyojulikana kama Birds in the Trap Sing McKnight (2016) ilikua ni albamu yake ya kwanza katika orodha ya albamu bora katika orodha ya Bilboard. Mwaka uliofuata alitoa albamu nyingine akimshirikisha Quavo ikiitwa Huncho Jack, Jack Huncho, chini ya kundi lililoitwa Huncho Jack. Mnamo mwaka 2018 alitoa albamu iliyoitwa Astroworld na kfranya wimbo wake wa "Sicko Mode" kushika namba moja katika orodha ya bilboard.


Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Travis Scott kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.