Nzige-jangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Nyongeza matini
Nyongeza matini
Mstari 72:
Bidhaa za [[udhibiti wa kibiolojia]] zimekuwa zikiendelewa tangu miaka ya mwisho ya tisini, haswa bidhaa zilizo na kuvu ya asili iliyo [[pathojeni]] wa wadudu (yaani kuvu inayoambukiza wadudu), ''[[Metarhizium acridum]]''. Spishi za ''[[Metarhizium]]'' zinaenea duniani kote na zinaambukiza vikundi vingi vya wadudu, lakini zinaonyesha hatari ndogo kwa [[binadamu|wanadamu]], [[mamalia]] wengine na ndege. ''M. acridum'' inaambukiza tu panzi wenye [[kipapasio|vipapasio]] vifupi, kikundi ambacho nzige ni wana wake, na kwa hivyo imechaguliwa kama [[kiambato kiamilifu]] cha bidhaa hizo. Ni salama mno kwa sababu haitoi sumu kama hufanya spishi nyingine za ''Metarhizium''.
 
Bidhaa inayopatikana sasa katika Afrika na Asia ya Kati, inaitwa NOVACRID. Bidhaa nyingine, Green Muscle, iliyobuniwa katika mradi [[LUBILOSA]], ilipatikana hapo zamani lakini ikatoweka kutoka [[soko]] hadi hivi karibuni, wakati leseni ya uuzaji ilipewa [[kampuni]] nyingine. Bidhaa hizo zinatumika kwa njia ile ile kama dawa za kikemikali, lakini haziui haraka kama zile. Kwa vipimo vilivyopendekezwa kuvu inaweza kuchukua wiki mbili hadi tatu kuua hadi 90% ya nzige. Kwa sababu hiyo inashauriwa kutumiwa hasa dhidi ya tunutu. Hao hupatikana zaidi katika jangwa, mbali na maeneo ya mazao, ambapo kuchelewesha kwa kifo hailetei uharibifu wa mazao kwa kawaida. Faida ya bidhaa ni kwamba zinaathiri panzi na nzige tu, ambayo hufanya ziwe salama sana kuliko viuawadudu vya kikemikali. Hasa, inaruhusu maadui wa asili wa nzige na panzi kuendelea na kazi yao ya faida. Hao wanajumuisha ndege, [[nyigu kidusia|nyigu vidusia]] na mbuai, nzi vidusia na spishi fulani za mbawakawa. Ingawa maadui wa asili hawawezi kuzuia tauni, wanaweza kupunguza marudio ya milipuko na kuchangia udhibiti wao. Dawa za kibiolojia zinapendekezwa hasa kutumika katika maeneo ya mazingira nyeti kama [[hifadhi ya kitaifa|hifadhi za kitaifa]] au karibu na [[mto|mito]] na miili mingine ya maji.
 
==Picha==