Kilatini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 33:
 
==Kilatini cha kisasa==
Kilatini kilikuwa na upanuzi mkubwa kuanzia karne ya 16; misingi ya sayansi ya kisasa ilijadiliwa katika Ulaya kwa Kilatini kilichokuwa lugha ya vyuo vikuu kote Ulaya. Katika karne ya 18 na 19 mataifa mengi yalianza kuimarisha lugha zao na kuzitumia kwa ngazi zote za elimu. Lakini wataalamu wa Ulaya na Marekani waliendelea kutumia majina ya Kilatini kwa kutaja habari za kisayansi na kubuni majina mapya kufuatana na kanuni za Kilatini kwa kutaja vitu na viumbe vilivyotambuliwa na kuelezwa kisayansi. Kazi hii iliendelea hata wakati matumizi ya Kilatini kama lugha ya kujadiliwa yalishafikia mwisho wake.
 
Katika karne ya 20 kulikuwa na harakati ya wapenzi wa lugha kuunda misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, [[mtandao]] n.k. [[Wikipedia ya Kilatini]] ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka [[2019]].