Kihindi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d kuondoa kiungo cha ramani using AWB
2001,ukoloni,1945
 
Mstari 1:
'''Kihindi''' ([[Devanagari]]: हिन्दी au हिंदी) ni [[Lugha za Kihindi-Kiulaya|lugha ya Kihindi-Kiulaya]] nchini [[Uhindi]], [[Nepal]], [[Afrika Kusini]] na [[Singapuri]] inayozungumzwa na [[Wahindi]]. Ni lugha ya kitaifa nchini Uhindi. Mwaka wa [[2001]] idadi ya wasemaji wa Kihindi nchini Uhindi imehesabiwa kuwa watu milioni 258; tena kuna watu milioni 120 ambao huitumia lugha ya Kihindi kama lugha ya pili au ya mawasiliano. Wengine husema kwamba kinaeleweka kati ya theluthi mbili ya Wahindi wote yaani takriban watu milioni 650, na wasemaji wa Kihindi kama lugha ya kwanza ni zaidi ya milioni 180. Pia kuna wasemaji 361,000 nchini Afrika Kusini (2003), wasemaji 77,600 nchini Nepal (2011) na wasemahi 13,100 nchini Singapuri (2010). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kihindi iko katika kundi la Kiaryan au la [[lugha za Kihindi-Kiajemi]]. Lugha za karibu ni pamoja na [[Kipunjabi]], [[Kisindhi]], [[Kigujarati]], [[Kimarathi]] na [[Kibengali]].
 
Lugha imetoka katika [[Sanskrit]] ya kale iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.
 
==Kihindi, Kiurdu na Kihindustani==
Kihindi ni umbo la lugha ya [[Kihindustani]] nchini India. Kihindustani ilikuwa jina la pamoja katika Uhindi wa kaskazini kabla ya ugawaji wa mwaka [[1947]] mwisho wa [[ukoloni]] na kuanzishwa kwa nchi huru za [[Pakistan]] na India. Baada ya uhuru lugha ya pamoja ya awali iliitwa "Kihindi" upande wa India na "[[Kiurdu]]" upande wa Pakistan. Hali halisi lugha hizi mbili ni kama lugha 1 hata kama Urdu huandikwa kwa [[herufi za Kiarabu]] na Kihindi kwa herufi za [[Devanagari]].
 
==Viungo vya nje==