Bremen : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 23:
Mji una wakazi 546,000. Pamoja na eneo la jirani kuna watu [[milioni]] 2.37 katika [[mazingira]] ya Bremen.
 
Bremen ni [[dola-mji]] ikiwa moja ya [[Majimbo ya Ujerumani|majimbo 17]] ya kujitawala ya Ujerumani. [[Jina rasmi]] ni „Mji huru wa Hanse wa Bremen“ ([[Jimbo la Bremen|Freie Hansestadt Bremen]]). [[Hanse]] ilikuwa [[shirikisho]] la kimataifa la miji ya [[biashara]] iliyojitawala katika [[Zama za Kati|karne za kati]]. Kwa muda mrefu wa [[historia]] yake Bremen ilikuwa kama nchi ndogo ya kujitegemea hadi kujiunga na [[Dola la Ujerumani]] [[1871]]. [[Jimbo la Bremen]] lina miji miwili ya Bremen yenyewe na [[Bremerhaven]].
 
[[Wafanyabiashara]] wa Bremen waliwahi kuwa na biashara na [[nchi za nje]] kwa [[jahazi]] na [[meli]] zao tangu [[karne]] nyingi. Hata [[mawasiliano]] kati ya [[Afrika]] na Ujerumani yalipitia hasa Bremen na mji jirani wa [[Hamburg]].