Mitalojia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{jaribio}} '''Mitalojia''' ''(ing. metrology)'' ni ''elimu ya upimaji''<ref name=BIPM>{{cite web |title=''What is metrology?'' Celebr...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:02, 31 Mei 2020

Makala hiyo kuhusu "Mitalojia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Mitalojia (ing. metrology) ni elimu ya upimaji[1]. Inalenga kuweka msingi kwa maelewano kuhusu vizio na matumizi yake ambayo ni jambo la kimsingi kwa shughuli za kimataifa.

Jina

Neno limeundwa na "mita" (kipimo cha kimataifa cha umbali; kiasili Kigiriki μετρον) na "lojia", ambayo ni kiambishi inayotaja sayansi au elimu ya jambo fulani[2]

Asili

Asili ya sayansi ya upimaji ya kisasa ilipatikana wakati wa mapinduzi ya Kifaransa. Wakati ule uwingi wa vizio vya urefu vilivyokuwa kawaida, mara nyingi kwa kutumio vizio vya kimwili[3], Metrology is the scientific study of measurement. Hapa wataalamu walipendekeza kutumia kizio kilichorejelea chanzo cha kisasili yaani sehemu ya mzingo wa Dunia. Hii iliunda mfumo wa vizio vilivyokadiriwa kidesimali mnamo mwaka 1795. Mfumo huu ulianza kutumiwa pia na nchi nyingine na hatimaye kuleta mfumo wa vipimo sanifu vya kimataifa[4].

Matawi ya mitalojia

Wataalamu wa mitalojia huangalia hasa mambo matatu:[5][6] 1. Ufafanuzi wa vizio vya upimaji. Huu unahusu hasa kurejelea vizio vya upimaji kwa vizio vya kifizikia, tofauti na vizio vya kimazingira kama awali.

2. Kuhakikisha na kutathmini matumizi ya vizio hivi katika tasnia na biashara

3. Matumizi ya vizio vya upimaji katika sheria za nchi na za kimataifa.

Marejeo

  1. What is metrology? Celebration of the signing of the Metre Convention, World Metrology Day 2004. BIPM (2004). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2018-02-21.
  2. Kamusi ya KAST ilipendekeza istilahi "metalojia"; katika wikipedia hii tunatumia tahajia "mita", si meta; pia tunaona ugumu wa kufanana mno na istilahi ya Kiswahili kwa "metallurgy" (sayansi ya metali na aloi zao). Kwa namna nyingine umbo la Kiswahili ingekuwa pia "metrolojia", lakini hii imetumiwa tayari kama tahajia badala mojawapo wa elimu ya hali ya hewa (metorolojia). Tunakaribisha maoni kama tuache neno la kigeni na kubaki tu na "elimu upimaji"
  3. Kama vile futi, shibiri, wanda, ambavyo viko tofauti baina mtu na mtu, na vilisaninifishwa kieneo tu, kwa hiyo ilikuwa kawaida kukuta vizio tofauti kila mahali.
  4. Resolution 12 of the 11th CGPM (1960). Bureau International des Poids et Mesures. Jalada kutoka ya awali juu ya 14 May 2013. Iliwekwa mnamo 28 February 2017.
  5. Czichos, Horst; Smith, Leslie, eds. (2011). Springer Handbook of Metrology and Testing (2nd ed.). 1.2.2 Categories of Metrology. ISBN 978-3-642-16640-2. Archived from the original on 2013-07-01.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  6. Collège français de métrologie [French College of Metrology] (2006). Placko, Dominique, ed. Metrology in Industry – The Key for Quality. ISTE. 2.4.1 Scope of legal metrology. ISBN 978-1-905209-51-4. Archived from the original on 2012-10-23. ... any application of metrology may fall under the scope of legal metrology if regulations are applicable to all measuring methods and instruments, and in particular if quality control is supervised by the state.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)