Desibeli : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created by translating the page "Decibel"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:21, 31 Mei 2020

Desibel (kifupi dB, kutoka ing. decibel) ni kizio cha upimaji wa nguvu au ukali. Kinalinganisha vipimo viwili kwa kutumia logi

Matumizi yake ni hasa katika upimaji wa sauti na kaitka teknolojia ya umeme kwa kutaja nyongeza au kupungukiwa kwa volteji au sauti.

Kizio cha kimsingi ni "bel" na desibel ni sehemu yake ya kumi.

Nyongeza ya desibeli 3 inalingana takriban na kuzidisha nguvu mara mbili.

Kizio cha kimsingi cha bel kilipata jina lake kwa kumbukukbu ya Alexander Graham Bell aliyekuwa mmoja wa wabunifu wa simu.

Mara nyingi, desibeli hutumiwa kutaja ukubwa wa sauti kulingana na jinsi tunavyoisikia.

Decibel si kipimo sanifu cha SI .

Baadhi ya mifano ya sauti ni:

Kiwango cha Sauti Mifano
171 dB Karibu na bunduki kubwa ikipiga risasi
150 dB Karibu na injini ya ndege
110-140 dB Injini ya ndege kwa umbali wa mita 100
130-140 dB Watu wengi huanza kuhisi maumivu
130 dB Baragumu (umbali wa nusu mita)
120 dB Tarumpeta ya Vuvuzela (kwa umbali wa mita 1), hatari ya uharibifu wa sikio
80-90 dB Trafiki kwenye barabara kuu
60-80 dB Gari la abiria
40-60 dB Mazungumzo ya kawaida
20-30 dB Chumba tulivu sana
10 dB Jani kung'aa, kupumua kwa utulivu
0 dB Sauti ndogo kabisa inayosikika karibu na sikio

Marejeo