Mbege : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d #WPWP,#WPWPTZ
d #WPWP,#WPWPTZ
Mstari 2:
'''Mbege''' ni pombe ya asili ya [[Wachagga]], wakazi wa mkoa wa [[Mkoa wa Kilimanjaro|Kilimanjaro]]. Mbege hutengenezwa na [[ndizi]] mbivu, [[ulezi]], na [[maji]]. Mara nyingi mbege hutengenezwa na wanawake na hutumika katika sherehe na matukio mbalimbali kama vile harusi, misiba, [[ubarikio]], kuzaliwa kwa mtoto, n.k. Mbege hutumiwa pia kama faini kwenye mahakama za jadi. Utengenezaji wa mbege hufanywa pia kama shughuli ya kibiashara. Mbege huuzwa katika vilabu vya pombe na pia majumbani.
 
==AsilɪAsili==
Pombe hii hutengenezwa kwa kuchemsha ndizi mbivu kama vile [[ndizi songea]], [[ndizi uganda]],kibungara,kisukari(kama zinapatikana kwa sana) n.k. Ndizi hizo zikishachemshwa huachwa kwa kipindi cha kama tatu au zaidi ili zichache. Baada ya hapo unga wa ulezi hupikwa na kuachwa upoe. Ndizi zilizochemshwa na kuchacha huchanganywa na maji kisha kukamuliwa ili kupata juisi yake. Juisi hiyo huchanganywa na unga wa ulezi uliopikwa na tunapata (kivuo, kifue, togwa) na kuachwa usiku mzima. Kesho yake mbege huwa tayari kwa kunywewa.