Hagia Sophia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
[[Picha:Ayasofya-Innenansicht.jpg|thumb|200px|Hagia Sophia kwa ndani]]
[[Picha:00058 christ pantocrator mosaic hagia sophia 656x800.jpg|thumb|200px|Mozaiki ya Yesu katika ukuta wa Hagia Sophia]]
'''Hagia Sophia''' ni [[jina]] la [[Kigiriki]] ('''Ἅγια Σοφία''', yaani ''("Hekima takatifu"; kwa [[Kituruki]] Ayasofya) la [[kanisa]] kubwa mjini [[Istanbul]] - [[Konstantinopoli]] lililobadilishwa kuwa [[msikiti]] tangu [[mwaka]] [[1453]] isipokuwa lilipofanywa [[makumbusho]] miaka [[1934]]-[[2020]].
 
==Historia==
[[Ujenzi]] wa kanisa hilo ulianza mwaka [[532]] kwa [[amri]] ya [[Kaisari]] [[Justiniani I]] [[mtawala]] wa [[Roma ya Mashariki]] au [[Ufalme wa Byzanti]]. Alitaka kuwa na kanisa kubwa kuliko yote [[duniani]] akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa [[ukumbi]] mkubwa duniani hadi mwaka [[1520]]. [[Jengo]] lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justiniani alipoingia mara ya kwanza aliita, "Suleimani, nimekushinda", akimfikiria [[mfalme]] [[Suleimani]] wa [[Israeli ya Kale]] aliyejenga [[hekalu la Yerusalemu]].