Kontena : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 37 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q187956 (translate me)
Mstari 9:
 
==Tofauti zilizotokea kwa matumizi ya kontena==
Kabla ya kupatikana kwa kontena meli kubwa ilijazwa mizigo yake kwa msaada wa wafanyakazi mamia waliobeba bidhaa gunia kwa gunia ndani ya meli na kuzipakiza katika chumba cha mizigo. Bidhaa ziliwekwa katika magunia au katika masanduku yaliyotengenezwa kwa ubao kwa kila aina ya mzigo[[shehena]]. Zilijazwa katika malori au mabehewa ya mizigo ya reli, kupelekwa bandarini na hapo kuondolewa katika lori au kwenye behewa na wafanyakazi waliojaza nyavu iliyovutwa na winchi kubwa hadi kwenye meli. Hapa nyavu ulifunguliwa na wafanyakazi walichukua yale magunia au masanduku na kuzipanga katika nafasi za kubeba mizigo. Wakati meli ilifika bandari nyingine kazi ilirudia: wafanyakazi wengi walihitajika kubeba bidhaa kutoka vyumba vya meli, kuzipanga katika nyavu zilibebwa kwa winchi hadi nje ya meli, halafu hapa kusambazwa na wafanyakazi juu ya malori au mabehewa ya usafiri; mara nyingi kwanza hadi ghala ya bandarini na baadaye baada ya kuzipakia tena kwenye usafiri wa nchi kavu hadi mahali palipotakiwa.
 
Kontena ilibadilisha mtindo huu. Sasa bidhaa zinaingizwa katika kontena kiwandani au kwenye ghala. Kontena inahamihswa juu ya lori au behewa ya treni inayoisafirisha hadi bandarini. Hapa kuna winchi kubwa inayochukua kontena yote na kuiwekea juu ya meli. Kwenye bandari ya kufika kontena yote inapelekwa bandarini, moja kwa moja juu ya lori. Sasa ni watu wachache tu wanaoshughulika mzigo huu, na kazi inaendelea haraka zaidi pia kwa gharama dogo kuliko zamani.