Tetemeko la ardhi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 37:
Hali ya [[magma|mwamba huo ulioyeyuka wenye joto mno]] ndani ya dunia unafanana na hali ya sufuria ya maji ya kuchemka. Katika sufuria tunaona mwendo fulani, na tukiweka jani kwenye maji tunaona jinsi linavyozunguka pamoja na maji ambayo yanachemka. Maana ndani ya kiowevu kinachochemka kuna mwendo. Mwendo kama huo unapatikana pia kwenye mwamba ulioyeyuka ndani ya Dunia. Hivyo gamba la nje linaathiriwa na mikondo ndani ya mwamba ulioyeyuka, na mikondo yake. Kwa sababu ya kusukumwa, gamba huvunjika. Kwa hiyo badala ya pande moja zima la gamba, kuna baadhi ya [[Bamba la gandunia|mapande makubwa ya gamba]] yanayosogezwa yakiwa na kani kubwa.
 
[[Picha:Quake_epicenters_1963-98_notitle.png‎|right|370px450px|thumb|Ramani inayoonyesha mahali duniani ambapo nishati ya matetemeko ya ardhi iliachiwa baina ya miaka 1963 na 1998. Kila nukta inaonyesha kitovu cha tetemeko moja.]]
 
Katika baadhi ya sehemu za Dunia, mapande hayo yanakutana yakisukumana. Wakati huo, nguvu kubwa mno inasukuma mwamba thabiti wa gamba kuelekea juu na chini. Ndivyo hivyo baada ya miaka mingi sana, safu za milima zinavyojengwa. Pia pande moja linaposukumwa chini ya pande jingine, bonde kubwa sana linajengwa. Kwa mfano, kuna ufa mkubwa sana uliopo chini ya bahari, katika pwani ya [[California|Kalifornia]] magharibi mwa Marekani. Karibu na pwani ya nchi zilizopo katika pwani ya magharibi ya bara la [[Amerika]], kuna milima mingi kutokana na pande hilo kusukumwa juu. Pia, karibu na pwani, kuna mifereji ambapo chini ya bahari imekwenda chini sana, kwa ajili ya pande jingine lililosukumwa chini.