Tumaini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q190507 (translate me)
No edit summary
Mstari 1:
{{Maadili ya Kimungu}}
'''Tumaini''' ni hali ya [[nafsi]] yenye matarajio mema kuhusu mambo yajayo.
 
Katika [[dini]] tumaini linatokana hasa na [[imani]] katika [[wema]] wa [[Mwenyezi Mungu]].
 
==Katika Biblia==
[[Ukristo]], ukimfuata [[Mtume Paulo]], unaliorodhesha pamoja na imani na [[upendo]] kati ya [[maadili]] yanayodumu.
[[Ukristo]], ukimfuata [[Mtume Paulo]], unaliorodhesha pamoja na imani na [[upendo]] kati ya [[maadili]] yanayodumu. “Hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu” ([[1Thes]] 1:3). “Sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu” (1Thes 5:8). “Sikuzote tukiwaombea, tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote, kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni” ([[Kol]] 1:3-5). “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo” ([[1Kor]] 13:13).
 
Hayo matatu yanaitwa [[maadili ya Kimungu]] kwa kuwa [[asili]] na lengo lake ni [[Mungu]] mwenyewe. Hatuwezi kujipatia hayo, bali tunamiminiwa naye kwa pamoja tuweze kumsadiki, kumtumaini na kumpenda inavyotupasa tuwe [[Rafiki|marafiki]] wake. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu” ([[Ef]] 2:8). “Ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana” (1Thes 4:9).
 
Imani inatuletea tumaini na upendo kwa sababu tukipokea [[ufunuo]] wa Mungu na kumjua alivyo mwema, tunamtamani na kumtegemea ili tumpate milele, na tunavutiwa kumrudishia upendo. Hivyo imani inachanua tumaini na kuzaa upendo: hapo ni hai na kutuokoa. “Katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo” ([[Gal]] 5:6).
 
Tumaini ndiyo msimamo wa [[utashi]] wa kumlenga Mungu kama [[heri]] yake ya milele, kwa kutegemea ukuu wa wema ambao ameahidi kutusaidia. [[Abrahamu]] “aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa” ([[Rom]] 4:18). “Na tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu” ([[Eb]] 10:23). “Nani aliyemtumainia Bwana akaaibika?” ([[YbS]] 2:10).
 
Hata hivyo, hatuwezi kujua kama tutafika [[mbinguni]], ila tumaini linatupa hakika ya kwamba tunaelekea huko, na kwamba tukiendelea mpaka mwisho tutafika kweli. “Sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena.” (Rom 8:23-24). “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka” ([[Mk]] 13:13).
{{mbegu}}
[[Jamii:Saikolojia]]
[[Jamii:Dini]]