Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 16:
[[picha:Battle of tanga.jpg|thumb|250px|Mapigano ya Tanga]]
Hapo Waingereza waliamua kuchukua wanajeshi Wazungu kutoka Afrika Kusini chini ya amri wa jenerali [[Jan Smuts]] waliofika Kenya hadi mwisho wa 1915. Wakati huohuo Wabelgiji walipanga pamoja na Uingereza kupeleka vikosi vya jeshi lake la Force Publique katika Kongo mpakani wa magharibi.
 
Manowari [[SMS Königsberg]] ilikuwa Dar es Salaam wakati wa Julai 1914 ikaondoka bandarini na kushambulia meli za Kiingereza kwenye Bahari Hindi. Waingereza walijaribu kuizuia walituma manowari tatu HMS Astraea, HMS Pegasus na HMS Hyacinth kutoka Afrika Kusini kuelekea Dar es Salaam. SMS Königsberg ilianza kukosa makaa kwa injini yake ikarudi Afrika ya Mashariki; ilipopita Zanzibar ikakuta HMS Pegasus bandarini na kuizamisha. Königsberg ikakimbia ikajificha katika mdomo wa mto Rufiji. Waingereza walikusanya manowari kadhaa mbele ya mto Rufiji; manowari zao zilishindwa kuingia ndani ya mdomo wa mto lakini walivamia kisiwa cha Mafia na kuanzisha kiwanja cha ndege; hatimaye walifaulu kupiga Königsberg mara kadhaa na kusababisha uharibifu mkali hadi nahodha Mjerumani aliamua kuzamisha manowari yake mwenyewe kwenye tarehe 11 Juni 1915. Mabaharia Wajerumani walitoa mizinga yao na kuipeleka kwenye nchi kavu wakajiunga na Schutztruppe.
 
==Awamu ya pili: shambulio dhidi ya Tanganyika==