Nyenje-miti : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
Nyongeza aya
 
Mstari 34:
 
Mdudu mpevu ana urefu wa jumla wa [[sm]] 2 hadi 5 katika takriban spishi zote, ingawa mkubwa kabisa, [[nyenje-malkia]] (''Megapomponia imperatoria''), ana urefu wa mwili wa karibu na sm 7 na upana wa mabawa yake ni sm 18-20. Nyenje-miti wana macho yaliyotokeza na kubaidika sana kwenye pande za kichwa. Vipapasio vifupi vimetokeza kati ya macho. Pia wana [[oseli]] ndogo tatu zilizopo juu ya kichwa kwenye [[pembetatu]] kati ya macho mawili makubwa. Hiyo inatofautisha nyenje-miti na wana wengine wa Hemiptera. Sehemu za kinywa zinaunda [[rositro]] ([[w:rostrum (anatomy)|rostrum]]) ndefu na kali wanayoingiza katika [[mti]] au [[mmea]] ili kujilisha. Chini ya [[labro]] ([[mdomo]]) kuna muundo mkubwa kama [[pua]] ulio sehemu kubwa ya mbele ya kichwa. [[Msuli|Misuli]] ya kufyonza imo ndani yake.
 
[[Toraksi]] ([[kidari]]) ina pingili tatu na ina misuli yenye nguvu ya mabawa. Ina jozi mbili za mabawa kama viwambo yanayoweza kuwa mangavu au yenye [[mavundevunde]] au [[rangi]]. [[Vena]] za mabawa hutofautiana kati ya spishi na zinaweza kusaidia katika kitambulisho. Pingili ya tatu ya toraksi ina jozi ya [[operkulo]] ([[w:operculum (animal)|operculum]]) upande wa chini ambazo zinafunika [[timpano]] ([[w:tympanum (anatomy)|tympanum]]) na zinaweza kupanua upande wa nyuma na kuficha sehemu za [[fumbatio]]. Hiyo ina pingili ambazo zile za nyuma zina [[viungo vya uzazi]] ndani yao, na kwa majike ina kwenye ncha yake [[oviposito]] kubwa iliyo na makali kama [[msumeno]]. Pingili ya kwanza ya fumbatio inabeba jozi ya timpano, viwambo ambavyo vinakamata sauti. Kwa madume kuna aina mbili zaidi za viwambo: [[timbali]] ([[w:tymbal|tymbal]]) zinazofunikwa kwa kunyanzi linalotokana na pingili ya pili ya fumbatio, na viwambo vilivyokunjwa, aina zote mbili chini ya operkulo. Timbali zinafanywa kutetemeka na msuli wa timbali na kwa hivyo hutoa sauti. Kisha sauti huongezewa na kifuko cha [[hewa]] ndani ya mbele ya fumbatio ambacho hutumika kama [[chumba]] cha kuvuma.
 
==Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki==