Saratani ya mlango wa kizazi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''"Saratani ya mlango wa kizazi"''' ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi. Saratani...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 03:22, 16 Septemba 2020

"Saratani ya mlango wa kizazi" ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi. Saratani ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni:

  • Kutoka na damu isiyo ya hedhi ukeni.
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
  • Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokoma hedhi.
  • Kutoka damu iliyochanganya na majimaji ya uke.
  • Matone ya damu kutoka au damu kutoka kipindi ambacho si cha hedhi.
  • Kutokwa na majimaji au uchafu ukeni wenye harufu mbaya wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu.
  • Kusikia maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni.
  • Kukojoa mkojo wenye damu.
  • Kupitisha mkono na haja kubwa ukeni na wakati mwingine,
  • Upungufu wa damu.

Shingo ya kizazi ni nini?

Shingo ya kizazi ‘cervix’ ni sehemu ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo;

  • Kupitisha mbegu za kiume

kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi ili kupevusha yai,

  • Kupitisha damu ya hedhi
  • Mlango anaopitia mtoto wakati

wa kuzaliwa. Chanzo cha saratani ya kizazi husabishwa na Husababishwa na aina ya virusi kinachoitwa ‘Human Papilloma Virus’ (HPV), kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi.

  • Kuna tabia au hali hatarishi ambazo zinachangia mtu kupata saratani ya shingo ya kizazi, tabia/vitu hivyo ni

pamoj ana;

  • Kuanza ngono katika umri mdogo

(chini ya miaka 18).

  • Uvutaji wa sigara.
  • Kuwa na wapenzi wengi au

kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi.

  • Matumizi ya mafuta mengi

kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

  • Kutokula mboga za majani na

matunda.

  • Upungufu wa kinga mwilini.

Marejeo