Mlimbo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
dNo edit summary
 
Mstari 7:
'''Mlimbo''', '''mrimbo''' na '''mlimbolimbo''' ni majina yanayotumika kwa [[mti|miti]], [[kichaka|vichaka]] na [[mtambaa|mitambaa]] inayotoa utomvu unaonata ([[ulimbo]] au urimbo) na unaoweza kutumiwa ili kuzalisha aina ya [[mpira (dutu)|mpira]]. Kwa sababu ya hii [[spishi]] kadhaa huitwa [[mpira]] pia.
 
Hapo awali jina mlimbo lilitumika kwa spishi kadhaa za mitambaa kama zile za [[jenasi]] ''[[Landolphia]]'' na ''[[Saba]]''. Utomvu wenye kunata wa [[mmea|mimea]] hii mara nyingi ulitumika kukamata [[ndege (mnyama)|ndege]] wadogo hadi wa ukubwa wastani. Ni vivyo hivyo kwa spishi fulani za ''[[Euphorbia]]'' zinazoitwa mlimbolimbo, k.m. ''[[Euphorbia cuneata|E. cuneata]]''. Walakini, ulimbo uliotengenezwa kutoka kwa mlimbolimbo mwingine, ''[[Cassine aethiopica]]"'', unaandaliwa kutoka kwa [[jani|majani]] yake.
 
Hivi majuzi jina mlimbo limeanza kutumiwa kwa spishi za [[kimelea-nusu|vimelea-nusu]] katika [[familia (biolojia)|familia]] ya zamani [[Viscaceae]], ambayo sasa imeingizwa ndani ya [[Santalaceae]]. Katika spishi hizi utomvu unaonata hauzalishwi katika [[shina]] na [[tawi|matawi]] lakini katika [[tunda|matunda]] na hautumiki kukamata ndege. Unafanya mbegu kunatika kwenye domo la ndege wanaokula mbegu hizi. Ili kuziondoa ndege hutakiwa kupangusa domo lao kwenye mashina ya miti. Ikiwa mti ni wa spishi sahihi, basi mbegu huota na [[kimelea]] hulowea mti huo. Inapendekezwa kutumia [[mlimbo maridadi]] kwa vimelea-nusu vya familia inayohusiana [[Loranthaceae]]. Mimea hii hutoa idadi kubwa za [[ua|maua]] yenye [[rangi]] kali.